#TumiaVPN: Jinsi Ya Kutumia VPN na Ushauri Ipi Ni Bora Zaidi

Kwa tafsiri nyepesi, VPN inakuwezesha kuficha uwepo wako mtandaoni. Unaweza kujiuliza “kwanini nifiche uwepo wangu mtandaoni,” pengine kwa kutojua kuwa “hata ukiwa si mtu muhimu, bado mamlaka zinakufuatilia ili kujiridhisha huzisumbui.”

Lakini pia VPN inakuwezesha kutembelea tovuti zilizozuiwa na mamlaka, kwa mfano kuna wakati posts zangu kwenye machapisho yangu mbalimbali huzuiwa na wahuni wa Idara ya Usalama wa Taifa kwa ushirikiano na wahuni wenzao wa TCRA. Lakini VPN inafanya uhuni wao usiwe na maana.

Jinsi ya kutumia VPN ni rahisi. Kama simu yako ni Android basi nenda Play Store kisha search "VPN." Endapo unatumia iPhone, nenda App Store. Utaona VPN kibao. Ukihitaji ushauri kuhusu ipi bora, nishtue. Install kisha open, fuata maelekezo ya kujisajili. Na ukisha-login, hakuna kitengo wala TCRA wa kujua upo mtandaoni.

VPN ipi ni bora zaidi? Jibu fupi ni kwamba inategemea mapendezeo yako. Jibu refu ni kwamba binafsi nimekuwa nikitumia WINDSCRIBE kitambo sasa, na moja ya sababu kuu ni usalama wake (naam, sio kila VPN ni salama hususan za bure).

Lakini kubwa zaidi ni kwamba WINDSCRIBE inatoa allowance ya 10GB bure kwa mwezi (sio bando). Na unaweza kuongeza hadi 15GB kwa kufuata maelekezo yao. Unaweza kujiunga HAPA.

Ndimi jasusi wako,

Evarist Chahali