[#TumiaVPN] Jasusi Wako Amekuwa Akitahadharisha Kuhusu Usalama Wa Lissu TZ. Na Sasa Mwanasheria Wa Ughaibuni wa Mwanasiasa Huyo Aiandikia Serikali Kuhusu Suala Hilo

Jasusi wako ametanabaisha mara kadhaa kuwa hadhani kuwa ni salama kwa Mheshimu Tundu Lissu kurudi Tanzania muda huu. Hapana, simaanishi asitudi nyumbani kugombea urais wala simaanishi aishi huku ughaibuni milele. Ninachoeleza ni mtazamo wangu sio tu kama “jasusi” bali mtu ambaye “naishi roho mkononi.”

Jana nimeona twiti ya wakili wa Lissu akirejea kitu hicho hicho nilichoongea mara kadhaa kama zinavyoonyeshwa twiti hizo hapo chini. Lakini kwanza angalie twiti ya mwanasheria huyo wa Lissu na barua aliyoandika.

Waweza kusoma barua kamili HAPA.

Baadhi ya twiti za jasusi wako ni kama ifuatavyo

Nafsi inakataa kuamini kuwa Lissu atakuwa salama lakini mwisho wa siku suala hilo ni lake binafsi

Nakutakia Jumapili njema na kukualika kwenye kozi hii ya bure kwenye Jarida la Ujasusi

Jiunge leo HAPA

Ndimi jasusi wako,

Evarist Chahali