[#TumiaVPN] Episode Nyingine Ya #ZoomNaZu: Zuhura Anawahoji Watoto Hawa Wenye Vipaji Maalum - mtunzi wa vitabu, mshairi na mchoraji.

Katika 'Zoom na Zu' gumzo lilikuwa baina ya Zuhura Yunus na watoto wenye vipaji wote wakiwa jijini Dar es Salaam. Watoto hao licha ya kuwa na umri mdogo lakini wana uwezo wa kufanya mambo makubwa. Nao ni Tumaini John George ambaye ni mshairi, Edriss Mavura, mwandishi wa vitabu na Pearl Mavura, mwenye kipaji cha uchoraji.