[#TumiaVPN] Dear Mama Samia, Ulikuwa Mhanga wa Ukatili wa Magufuli Kabla Ya Lissu. Leo Wewe Wa Kuongea Upoloto Huu Kuhusu Jaribio La Kumuua Lissu? Shame On You!

Mhagalle Blog: MAKAMU WA RAIS SAMIA AMTEMBELEA LISSU

Sikuwahi kudhani kama kuna siku ningelazimika kusimulia unyama aliofanyiwa huyu mama kwa sababu deep in my heart nilimuona kuwa ni mwanasiasa mstaarabu, ambaye mazingira tu yamemlazimisha kuwa makamu wa Magufuli, Rais katili asiyethamini uhai wa mwanadamu.

Lakini kwa uhuni huu aliofanya huyu mama kwenye kampeni, bora tu kuweka ukweli hadharani hata kama MATAGA watakanusha. Kukanusha ukweli hakuufanyia kuwa uongo.

Huenda kuna baadhi ya watu hamjasikia alichoongea huyu mama. Msikilize hapa

Huwezi kuamini kuwa mnafiki huyu ndiye huyu hapa chini akiongea na Lissu alipokuwa Nairobi kwa matibabu

Lakini hawa ndio CCM. Ni kama chama cha wachawi ambacho hata yule anayeonekana muungwana, ipo siku ya siku ataonyesha rangi yake halisi.

Nasikia majuzi Lissu alipofanya mkutano wake wa kampeni Mbagala, mwanasiasa mmoja wa CCM, kijana anayesifiwa kwa “kuendesha siasa za kistaarabu,” alitwiti picha ya mkutano wake uliofanyika Mbagala miaka ya nyuma, yaani kama kuonyesha kuwa yeye alipata watu wengi kuliko Lissu. Ovyo kabisa.

Lakini wa ovyo kabisa ni wafuasi wa vyama vya upinzani ambao hata Bashite akiongea maneno matamu kwao, watamuona shujaa. Tumeshuhudia haya kwa kina Nape na wazushi wenzie ambao wakiwa kwenye chama chao wanauma, wakiwa mtandaoni wanapuliza, na wazembe wa kutanzua mambo wanawashangilia.

Turudi kwa huyo mama, huenda wengine mshawahi kuskia mkasa huu uliomkumba mwanzoni tu mwa utawala wa Magufuli. Ni kwamba, Magufuli alikuwa paranoid kuwa huyo mama alikuwa anatumiwa na Jk ili kumwondoa yeye Magufuli. Kama ni kweli au la, wanajua wenyewe.

Lakini kutokana na kunyanyaswa kupindukia, huyo mama akatishia kujiuzulu. Kosa!

Magufuli kama mwanasiasa katili asiye na huruma, akamfanyizia huyo mama kitu mbaya sana. Lakini sio mwanasiasa katili tu, bali Magufuli ni mtu anayependa kunyanyasa wanawake, na uthibitisho upo kwenye “mautani yake yanayokera” kuhusu wanawake, katika hotuba zake mbalimbali.

Kwa kifupi, bila kuingia kwa undani, Magufuli aliagiza vijana wake wamrekodi huyo mama “kwenye faragha zake,” kisha akaitwa na kuonyeshwa kilichorekodiwa. Akaambiwa ajiuzulu aone kitakachomtokea. Akafyata mkia. Mpaka leo. Hii ilitokea takriban mwaka mmoja kabla Lissu hajamwagiwa risasi katika jaribio la mauaji lililokuwa na baraka za Magufuli.

Sasa kumsikia huyu mama anaongea upoloto kuwa sijui polisi wa CCM wakimkosa mtu kwenye risasi tatu inabidi wawajibike, ni wazi kuwa labda wmechimbiwa tena mkwara na Magufuli au labda “alielemewa na kinywaji yake pendwa.”

Ni kwa sababu tu wapinzani wetu wanaendesha siasa za kistaarabu lakini huyu mama anaishi kwenye nyumba ya vioo, na hapaswi kabisa kuingia kwenye siasa za kuchafuana. Watu wana data zake chafu, lakini wamekuwa wakimstahi kwa sababu

(a) Watu wengi wamekuwa wakidhani kuwa ni mwanasiasa mstaarabu

(b) Wanaojua yanayomsibu katika huo umakamu, wanamuonea huruma kwa sababu ni kama mateka wa Magufuli.

Mwaka jana tu kulipatikana taarifa kuwa aliwekewa sumu na “watu wasiojulikana,” na ilikuwa almanusra aondoke. Hawezi kujiuzulu kwa sababu bado anakumbuka vizuri hilo tishio alilopewa na Magufuli.

Baadhi yetu tunaamini bila shaka kuwa huyo mama anatamani Magufuli “aondoke kwa namna yoyote ile” ili aweze “kuwa huru.”

Kwahiyo, pengine hata hayo maneno ya kichawi aliyoyaongea Mbagala yalikuwa maagizo aliyopewa na Magufuli, kwa sababu huyu mama si mtu wa kuongea upoloto wa aina hiyo. However, until proven innocent, she remains guilty as charged by court of public opinion.

Nihitimishe kwa kusisitiza umuhimu wa dua/sala mfululizo dhidi ya huyo dikteta, kwa sababu japo bado kuna imani kuwa hatofika Oktoba 28, lakini dozi ya dua/sala ni muhimu isipungue.

Jumapili njema!