Ticking Time Bomb: Kushamiri Kwa "Mahubiri Ya Dini vs Dini" Huko Instagram

Hii ni takriban video ya 10 nakutana nayo huko Instagram ambapo kunazidi kudhamiri maongezi ya kidini yanayolenga dini nyingine. Japo video hii ni ya kiongozi wa dini ya Kiislamu, trend niliyobaini huko Instagram inajumuisha pia viongozi wa dini wa Kikristo pia.

Mambo haya yalishamiri sana zama za Mzee Ruksa, lakini yakafifia baadaye kabla ya kuibuka kwa kasi zama za Jk, yakafifia na sasa yanaelekea kurudi tena.

Chonde chonde Watanzania wenzangu, tujitahidi tuwezavyo kukemea namna yoyote ile inayopandikiza chuki za kidini.

Najua kuna watakaokerwa na tahadhari hii lakini ukweli shurti usemwe, na kuuchukia ukweli hakuufanyi kuwa uongo.