Tathmini ya kiintelijensia ya miaka miwili ya urais wa Mama @SuluhuSamia
Leo Machi 19, 2023, Rais Samia Suluhu anatimiza mwaka wa pili wa urais wake. Siku kama ya leo, mwaka jana ambapo Rais Samia alitimiza mwaka mmoja wa urais wake, Jasusi aliandika uchambuzi wa kina kuadhimisha siku hiyo.
Na leo Jasusi anatekeleza tena kwa ufanisi jukumu hilo. Katika tathmini ya mwaka wa pili wa uongozi wa Rais Samia, kunafanyika ulinganifu katika ya mwaka mmoja wa Rais Samia dhidi ya utawala uliomtangulia, mwaka wa pili dhidi ya mwaka wa kwanza, na kisha kubashiri mustakabali wake.