Tathmini ya kiintelijensia: Mbowe ajipa masaa 48 kufanya maamuzi magumu, je atagombea au la? Vyovyote atakavyoamua, je mustakabali wa Chadema utakuwaje
Jana Disemba 18, 2024, Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Mheshimiwa Freeman Mbowe aliongea na wageni mbalimbali waliomtembelea nyumbani kwake ambao kwa mujibu wa maelezo waliwasilisha ombi la kumtaka agombee tena nafasi hiyo.
Hata hivyo, Mheshimiwa Mbowe alieleza kwamba amepokea ombi hilo na atatumia masaa 48 kabla ya kutoa tamko rasmi endapo atagombea au la. Anatarajia kufanya hivyo kwenye mkutano na wahariri wa vyombo vya habari utakaofanyika keshokutwa.
Pamoja na mambo mengine, tathmini hii ya kiintelijensia inajikita kwenye mambo yafuatayo
Je atagombea au la?
Faida na hasara za kugombea
Faida na hasara za kutogombea
Mustakabali wa Chadema bila kujali Mheshimiwa Mbowe atagombea au la