Tathmini ya kiintelijensia kuhusu ziara ya Rais Kagame nchini Tanzania Aprili 27 - 28, 2023
Rais Paul Kagame wa Rwanda leo April 27, 2023 anaanza ziara ya siku mbili nchini Tanzania.
Hii ni ziara ya pili ya Rais Kagame nchini Tanzania tangu Rais Samia aingie madarakani, ambapo ziara yake ya kwanza ilikuwa Desemba 2021 alipohudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru wa Tanzania.
Pamoja na mambo mengine, tathmini hii ya kiintelijensia inajenga picha pana ya ziara hiyo ikiwa ni pamoja na mahusiano ya Tanzania na Rwanda chini ya tawala tatu - utawala wa Rais Kikwete, marehemu Magufuli na sasa Rais Samia, uhusiano mbovu kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, uwepo wa majeshi ya Rwanda (na Tanzania) nchini Msumbiji, na nafasi ya Rwanda barani Afrika na kimataifa.