Tathmini ya kiintelijensia kuhusu onyo la IGP Wambura dhidi ya "wenye mpango wa kuipindua serikali ya Rais Samia"
Jana Ijumaa ya Agosti 11, 2023, Mkuu wa Jeshi la Polisi, Camillus Wambura alitoa onyo dhidi ya watu aliodai kuwa wanataka kuiangusha serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu.
Tathmini hii ya kiintelijensia inaangalia, pamoja na masuala mengine, endapo ni kweli kuna mpango wa kuipindua serikali ya Rais Samia Suluhu, na kama ni kweli, wahusika ni akina nani. Kadhalika, tathmini inatupia jicho athari zinazoweza kujitokeza endapo IGP Wambura “alikurupuka” kutoa tahadhari hiyo.