Tathmini ya kiintelijensia: Fursa na Changamoto kwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa Idara ya Usalama, Ndg Selemani Mombo [Sehemu ya Kwanza: FURSA]
Juzi, Rais Samia Suluhu alimteua Ndugu Selemani Mombi kuwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa Idara ya Usalama wa Taifa (DGIS) kuchukua nafasi ya Balozi Ali Siwa ambaye ilielezwa kwamba amestaafu.
Jasusi aliandika jana uchambuzi wa kiintelijensia kuhusu tukio hilo zito
Uchambuzi wa kiintelijensia kuhusu Rais Samia kumteua Mkurugenzi Mkuu mpya wa Idara ya Usalama wa Taifa, Selemani Mombo na kuchukua nafasi ya Balozi Ali Siwa
Jana Alhamisi ya Julai 11, Rais Samia alifanya mabadiliko ya TANO kwenye uongozi wa juu wa Idara ya Usalama wa Taifa, kwa kumteua na kumwapisha Ndugu Selemani Mombo kuwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa taasisi hiyo nyeti. Japo Watanzania wengi walipokea taarifa hiyo kwa mshangao, duru za kiintelijensia zilishaonyesha kuwa mabadiliko hayo yalikuwa sio suala la kama yangetokea bali lini yangetokea (not if but when)
Tathmini hii inaangalia FURSA (opportunities) na CHANGAMOTO (challenges) kwa DGIS Mombo katika wadhifa wake huo mpya.
TANGAZO
Kwa walio nje ya Tanzania, vitabu vinapatikana dunia nzima HAPA