Tathmini ya kiintelijensia: Baraza Kuu la Jumuiya za Ansaar Sunna Tanzania (BASUTA) latetea mkataba wa bandari, lamsapoti Jk, na kulilaumu Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) kwa kupinga mkataba huo
Je Jk aliyekemea "kuchanganya dini na siasa" baada ya tamko la TEC atawakemea BASUTA pia?
Jana Agosti 24, Baraza Kuu la Jumuiya za Ansaar Sunnah Tanzania (BASUTA) lililtoa tamko la kuunga mkono mkataba wa bandari sambamba na kumuunga mkono Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kwenye tamko lake la “kukemea kuchanganya dini na siasa” na wakati huohuo kulishutumu Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) lililopinga mkataba huo.
Kabla ya kuingia kwenye tathmini hii, soma tamko hilo la BASUTA