Tahadhari Kuhusu Matapeli Wanaopiga Simu Kisha Kuongea Lugha Isiyoeleweka, Ukiwapigia Simu Inakorofisha. Namba Mojawapo Ni 0620657747 (Halotel) Jina Sitta Nghabi Mbasha
Naomba nimnumkuu dadangu ambaye ametokewa na mkasa husika. Amenieleza kuwa amesikia pia watu wengine wakiwa wahanga wa uhuni huo ambao yaelekea unahusisha udukuzi wa simu husika
Kuna huu mtindo umeingia mtu anakubip mara nyingi mpaka unaamua kumpigia au anakubip mara moja kisha anakupigia halafu ukipokea anakuongelesha kwa lugha ambayo siyo kiswahili wala kiingereza (nahisi ni kabila mojawapo hapa Tanzania)
Ukiita halo tu anaanza kuongea kwa hiyo lugha kisha baada ya muda mfupi anakata simu
Ukimpigia tena anaongea lugha hiyo hiyo baada ya muda anakata
Ilimtokea binti yangu mara kadhaa kisha simu ikawa inasumbua inakuwa nzito na network inasumbua sana mara simu ina stuck mara inajizima na kuwaka yenyewe
Akai buck up na kuiset kwa settings za kiwandani ikakaa sawa
Kuna mtu akamwambia wadukuzi wa simu siku hizi wanafanya hivyo
Leo imenitokea mimi mtu kanipigia kwa namba ya mtandao wa halotel 0620657747 imesajiliwa kwa jina Sitta Nghabi Mbasha
Amebip sikuhangaika nayo
Baada ya muda mrefu akanipigia nilipopokea akaanza kuongea kwa lugha nisiyoielewa kisha akakata simu
Nilipomwambia binti ndio kanipa hiyo story
Ghafla simu yangu ikazima na kuwaka yenyewe
Nikaitafuta hiyo namba nikaiblock
Sasa hivi nataka nii buck up nifute kila kitu inanze upya