Taarifa Za Didier Mlawa Zaanza Kumininika. Ilikuwa Aingie Kitengo Mwaka 2000, Vetting Ikagoma Baada Ya Kugundulika Alikuwa Anatapeli Watu Akidai Yeye Usalama, Anadaiwa Na Houseboy Hajamlipa Hadi Leo

Majuzi niliweka rai kwa wanaomjua Didier Abdallah Mlawa aka Kigogo wawasilishe taarifa zake. Nafarijika kueleza kuwa taarifa zimeanza kumiminika. Kwa kuanzia ni taarifa hii niliyoipata jana usiku.

Mtoa taarifa alianza kwa kueleza kuwa anatoa taarifa kuhusu Mlawa kwa ajili ya kutikia wito wa Jasusi kwa jamii kwamba kila mwenye taarifa za haramia hiyo aziwasilishe.

Mtoa taarifa anasema alimfahamu Mlawa 2007. Alifahamia nae maeneo ya Makumbusho kwenye ofisi za Idara ya Usalama wa Taifa enzi hizo wakati baba ya mtoa taarifa akiwa afisa kabla hajastaafu miaka michache baadaye.

Mtoa taarifa anaeleza kwamba Mlawa alikuwa anaenda hapo ofisi za Usalama wa Taifa kumfuata dada mmoja anaitwa Fatma ambaye ni Afisa Usalama wa Taifa. Dada huyo alikuwa na mahusiano na Mlawa.

Aidha kupitia dada huyo au mtu mwingine, Mlawa alikuwa ajiunge na Idara ya Usalama wa Taifa intake ya mwaka 2000.Hata hivyo, vetting yake iligoma kwa sababu walihgundua mkuwa Mlawa alikuwa akijitangaza kuwa yeye ni Afisa Usalama wa Taifa ilhali si kweli. Na baada ya kubaini hilo, wakampiga chini. Uamuzi huo ulimuumiza sana Mlawa, na kila alipofika maeneo hayo na kuishia getini alikuwa anasema kwa uchungu na hasira kuwa “hapa pangekuwa ofisini kwangu...”

Mtoa taarifa anahitimisha kuwa anaamini kuwa hiyo ndio sababu ya chuki kubwa ya Mlawa kwa system. Kipindi hicho Mlawa alikuwa anaishi Sinza Palestine palepale kituoni kama unatoka Makaburini upande wa kushoto.

Pia alikuwa anafanya kazi maeneo ya Mikocheni ila ilikuwa ni ofisi ya wazungu (inawezekana ni huko ambako nako aliiba fedha na kutoroka kwa mujibu wa taarifa kuhusiana na wizi wake?)

Mtoa taarifa anaeleza pia kuwa huyo dada Fatma alikuja kumbwaga Mlawa baada ya yeye Mlawa kutoka na rafiki wa huyo dada, ambapo baadaye aliambiwa kuwa Mlawa alikuwa analalamika kuwa huyo Fatma hataki kuolewa nae ilhali si kweli. Dada huyo alihitimisha kuwa Mlawa ni tapeli tu anayewazunguka wanawake kwa ahadi za kuoa.

Hata hivyo, milima haikutani ila binadamu hukutana, huyo dada Fatma baadaye alikutana na Mlawa Dodoma ambapo Mlawa alikuwa anaishi Area D, na huyo dada alikuwa Dodoma kikazi Bungeni.

Mtoa taarifa anaeleza kwamba moja ya madhambi ya Mlawa huko Dodoma ni kwamba alimtelekea houseboy wake na hakumlipa hata senti tano hadi leo.

Baadaye Mlawa alidai anaondoka kwenye Ulaya sijui “ana safiri na Rais JK enzi hizo” kumbe ndo akawa anatoroka Tanzania.

Huyo dada Fatma ndio alipatwa uchungu na kulipa deni la houseboy ambapo yule dada anasema aliona huruma akalipa deni alilokuwa anadai huyo houseboy.

Naomba kumsihi yeyote mwenye taarifa zaidi aziwasilishe. Kila mtu mwema anapaswa kupambana kwa dhati kumtokomeza haramia huyo. Ofkoz umaarufu wake umeshuka, amebaki kujikomba Simba na huko CCM lakini nyoka anabaki kuwa hatari endapo hajaangamizwa. Kwa jitihada za watu wenu wasiotaka kuona maharamia wanatesa watu mtandaoni, basi yawezekana kabisa kumuangamiza maamuma huyo.