Taarifa ya uchunguzi wa kiintelijensia kuhusu mkakati wa kusambaza ushoga na usagaji 'kila kona ya Tanzania',
Usuli wa taarifa
Kwa mujibu wa sheria za Tanzania, vitendo vya ushoga na usagaji ni kinyume cha sheria. Hata hivyo, sheria hiyo ipo kinadharia zaidi kuliko vitendo, kwa sababu licha ya ushoga na usagaji kuzidi kushimiri nchini humo, hakuna rekodi angalau za hivi karibuni za watu waliochukuliwa hatua kwa kujihusisha na vitendo hivyo.
Kufuatia ripoti za kusambaa kwa vitendo vya ushoga na usagaji, Barua ya Chahali ilifanya uchunguzi wa kiintelijensia kufahamu, pamoja na mambo mengine, vitendo hivyo vimesambaa kwa kiasi gani - na kujiridhisha kuwa taarifa za kusambaa kwa vitendo hivyo hazichangiwi na kinachoonekana kama upinzani dhidi ya ushoga/mashoga na usagaji/wasagaji, kwa maana kwamba taarifa hizo hazikuzi ukubwa wa “tatizo” ili kushinikiza hatua dhidi ya “tatizo” husika - na kufahamu chanzo cha kusambaa huko.
Katika taarifa hii, “vitendo vya ushoga na usagaji” vitajumuishwa na kuitwa “ushoga” hasa kwa vile kwa Kiingereza, neno “homosexuality” linamaanisha “mapenzi ya jinsia moja”. Na kwa Kiswahili, mahusiano ya kimapenzi kati ya mwanaume na mwanaume huitwa ushoga ilhali yale kati ya mwanamke na mwanamke huitwa usagaji, japo kimsingi, kiujumla ushoga - kwa maana ya ushoga wa wanaume na usagaji wa wanawake - ndio hiyo homesexuality ya Kiingereza.
Licha ya kuonyesha “Tanzania imefikaje hapa ilipo kuhusiana na ushoga”, taarifa hii pia inaeleza kwa kina kuhusu mkakati wa kusambaza ushoga “kila kona ya Tanzania”, mbinu zinazotumika, na wahusika katika mkakati huo.
Historia ya ushoga nchini Tanzania
Japo ni vigumu kueleza kwa uhakika kuhusu historia ya ushoga nchini Tanzania, yayumkinika kutanabaisha kuwa suala ambalo limekuwa na mjadala mkubwa katika jamii ya Tanzania na ulimwenguni kwa ujumla. Historia ya ushoga nchini Tanzania imejaa changamoto, mizozo, na mchakato wa mabadiliko ya kijamii.
Katika jaribio la kuchunguza historia ya ushoga Tanzania, taarifa hii inaangalia vipindi vikuu vitanne:
Ushoga kabla ya ukoloni
Ushoga baada ya uhuru lakini kabla ya mageuzi
Ushoga baada ya uhuru baada ya mageuzi
Ushoga katika zama hizi