Sintofahamu kuhusu kipi kianze kati ya katiba mpya na tume huru ya uchaguzi yaendelea, Chadema wadai "Zitto ameafikiana nao kuanza na katiba badala ya tume huru", yeye ang'aka
Mada inayotawala mijadala ya vyama vikuu vya upinzani nchini Tanzania, Chadema na ACT-Wazalendo, ni suala la katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.
Kwa kifupi, msimamo wa Chadema ni kuanza na kudai katiba mpya kisha ndio ufuate mchakato wa kupata tume huru ya uchaguzi. Kwa upande wao, ACT-Wazalendo wanataka tume huru kwanza.
Makala hii fupi haitogusia saba…