#SimuliziZaJasusi: Swali linaloulizwa chinichini kwa miaka 23 tangu Nyerere atutoke - kifo chake kilikuwa mapenzi ya Mungu kweli au kulikuwa na mkono wa mtu/watu?
Simulizi Za Jasusi ni safu mpya katika kijarida hiki ambayo itakuwa ikikuletea simulizi zinazohusiana na masuala ya intelijensia. Jasusi ana mengi sana ya kukufahamisha, na ni matumaini yake kuwa kupitia safu hii ataweza kukupatia “access to” mgodi uliosheheni madini lukuki. Dhamira ni kuweka “simulizi” mpya kila wiki, lakini itategemea kama muda utaruhusu.
Pia Jasusi anaomba kutumia fursa hii kutanabaisha kuwa neno “simulizi” lina maana pana zaidi kuhusiana na safu hii. Miongoni mwa maana hizo ni kutolea maelezo mambo ambayo kwa sababu moja au nyingine yanafichwa au kuzuiliwa au yanatazamwa kama ni marufuku kufahamika kwa ninyi wenye nchi. Kadhalika, maana nyingine ya “simulizi” ni kuhusiana na ukweli, moja ya bidhaa zinazozidi kuwa adimu katika Tanzania yetu. Actually, katika Tanzania ya leo, kuwa “msema kweli” ni hatari zaidi kuliko kuwa muuza madawa ya kulevya.
And when is the best time kuzindua safu hii than today ambapo tunaadhimisha miaka 23 tangu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere afariki dunia, Oktoba 14, 2009?
Kichwa cha habari kinajieleza waziwazi. Kwa miaka 23 tangu kufariki kwa Nyerere, kumekuwa na swali linaloulizwa kimyakimya kama kifo chake kweli kilitokana na “mapenzi ya Mungu” au kulikuwa na “mkono wa mtu/watu”?
Jasusi anafahamu fika kuwa mada hii sio tu itawakera baadhi ya watu bali pia inaweza kuwaongezea hasira baadhi ya watu wanaoamini kuwa Jasusi nae alipaswa kuwa marehemu kitambo.
Makala hii, ya kwanza katika historia ya Tanzania, inatumia “jicho la kijasusi” kuchambua kifo cha Baba wa Taifa, sababu zilizopelekea kuibuka kwa swali la endapo kifo chake kilikuwa ni mapenzi ya Mungu au kulikuwa na mkono wa mtu/watu, na “relevance” ya maongezi haya kwa kuzingatia mazingira ya sasa, miaka 23 baada ya kifo cha Baba wa Taifa.