Siku 90 Za Mbowe Gerezani: Inasikitisha Mno Lakini Pia Inatafakarisha Sana.
Jana, Oktoba 19 ya mwaka huu, zimetimia siku 90 kamili tangu Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mheshimiwa Freeman Mbowe, akamatwe na kufunguliwa mashtaka ya ugaidi na uhujumu uchumi. SIKU TISINI.
Inasikitisha sana. Kwa sababu moja kubwa. Haki hupaswa sio tu kutendeka bali pia ionekane imetendeka. Sasa katika kesi hii ya Mheshimiwa Mbowe, sio tu kwamba haki h…