Siasa Za Makundi CCM: Kiongozi Mmoja wa Dini Na Mikakati Yake Dhidi ya Mama Samia
Taarifa za ndani ya chama tawala CCM zinaeleza kwamba kiongozi mmoja wa dini ambaye pia ana nafasi ya uongozi katika chama hicho yupo kwenye jitihada kubwa za kutanua upinzani dhidi ya Mama Samia.


Tafsiri ya twiti hiyo kwa Kiswahili ni kwamba kiongozi mmoja maarufu wa kidini ambaye pia ana wadhifa huko CCM ana mikakati kadhaa ya (a) kukwamisha urais wa Mama Samia (b) endapo hilo litafeli, basi kumzuwia Mama Samia katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2025.
Barua Ya Chahali haitomtaja kiongozi huyo wa kidini na kisiasa kwa sasa.
Kwa mujibu wa taarifa, kiongozi huyo “anatumika” na yeye pia ana “anaowatumia.” Katika kutumika, yeye kwa sasa ndio “sura ya hadharani” (public face) ya genge la kisiasa linalofahamika kama “Chato Gang.” Genge hili linaundwa na wanufaika wa utawala wa marehemu John Magufuli, na linapigana kufa na kupona kuhakikisha kuwa himaya iliyoanza kujengwa Kanda ya Ziwa inarudi kushika hatamu za uongozi.
Lakini pengine CCM isingefika hapa endapo ingezingatia tahadhari ambazo baadhi yetu tumekuwa tukitoa kitambo





Tanzania Updates @TanzaniaUpdates
PICHA: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na waumini wengine wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay leo ameshiriki Ibada ya Jumapili ya Familia Takatifu katika Kanisa hilo la jijini Dar es Salaam. https://t.co/13sUpmGjZp
Jasusi @Chahali
Askofu @jgwajima anakemea @usembassytz kuongelea suala la @freemanmbowetz kuvamiwa, lakini hajikemei yeye kama mtumishi wa Mungu kuvamia siasa. Kipi cha hatari zaidi kati ya tamko la ubalozi wa Marekani na viongozi wa dini kujigeuza wanasiasa? Dini + siasa = 💣 https://t.co/vZ1VqsLmJB


Tanzania Updates @TanzaniaUpdates
"Hivi karibuni kumekuwepo na tabia ya baadhi ya viongozi wa jumuiya kutumia mahubiri yao wakati wa ibada kuchambua masuala ya siasa kinyume na Katiba zao. Hakuna jumuiya iliyosajiliwa chini ya sheria ya jumuiya ili kufanya siasa" ~ K/Mkuu Mambo ya Ndani Meja Jenerali Rwegasira https://t.co/IVr0T6ikFo





Kama twiti hizo zinavyoonyesha, ni dhahiri CCM na serikali zake haiwezi kuja siku moja kulalamikia suala la kuchanganya dini na siasa kwa sababu yenyewe imekuwa ikiongoza jitihada za kutumia dini katika kufanya siasa zake.
Kimsingi, hata hivyo, ni muhimu kutambua kuwa both siasa na dini ni vitu vizuri vikitumika ipasavyo. Dini, kwa tafsiri nyepesi, ni mahusiano binafsi kati ya binadamu na mola wake (whatever that means to them). Na siasa, katika moja ya tafsiri zake nyingi, ni mahusiano kati ya mtu na dola. Kwahiyo, both dini na siasa vinamhusu mtu.
Hakuna tatizo kwa viongozi wa dini kuwakumbusha waumini wao kuhusu wajibu wao kama waumini. Na miongoni mwa waumini hao ni viongozi wa kisiasa. Kwahiyo, dini ikitumika vizuri, inaweza kutoa malezi mazuri kwa viongozi kisiasa ambao ni waumini wa dini husika. Unfortunately, kwa Tanzania yetu, it never works that way. Mara nyingi inakuwa kinyume chake, yaani viongozi wa kisiasa ndio wanaotoa mwongozo kwa viongozi wa dini.
Kibaya zaidi, miongozo hiyo hujikita kwenye maslahi binafsi ya viongozi hao wa kisiasa.

Na ndivyo ilivyotawala katika zama za marehemu Magufuli.
Viongozi wa kidini walikuwa na nafasi ya kipekee kwenye utawala wake, ambapo walipita huku na kule, baadhi yao wakikufuru na kudai “Magufuli ni chaguo la Mungu.”
Lakini pengine jambo la kukera zaidi na lililopaswa kukemewa mapema ni kitendo cha Magufuli kugeuza makanisa kuwa majukwaa ya kisiasa. Takriban kila Jumapili aligeuka mhubiri wa siasa makanisani.
Siku moja tunaweza kufahamu ni kwa jinsi gani kampeni za Magufuli dhidi ya ugonjwa wa korona zilivyochangia vifo vya maelfu ya Watanzania. Viongozi wa dini waliompa mwanasiasa huyo jukwaa la kuhubiri porojo zake nao wana damu mikononi mwao ya wenzetu waliokufa kwa korona kwa kuamini porojo hizo.
Uhusiano baina ya Magufuli na viongozi wa dini ulikuwa katika namna kwenye Baiolojia wanaita “symbiotic,” yaani uhusiano wa kutegemeana. Kwa upande mmoja, viongozi wa dini waliomnyenyekea Magufuli walipewa sapoti ya kifedha na upendeleo kwenye maeneo kama ya ulipaji kodi. Nao kwa upande wao, walimnufaisha Magufuli kwa kumtukuza kama “mungu-mtu” sambamba na kutumia nyumba zao za ibada kama majukwaa ya kisiasa kwa kiongozi huyo na chama chake.
Turudi kwa kiongozi huyo wa dini ambaye pia ni kiongozi wa CCM. Kama ilivyoelezwa awali, amekuwa akitumika kama “public face” ya Chato Gang. Unaweza kujiuliza, “anapata ujasiri huo? Je hahofii kufukuzwa huko CCM?”
Kwa upande mmoja, ujasiri wa kiongozi huyo unatokana na nguvu zilizo nyuma yake. Katika utumishi wake kwa taifa, hasa akiwa Waziri wa Ujenzi, Magufuli “alivuta” watu wengi wanaohusiana nae, mostly wa kabila lake. Na moja ya Wizara zenye “ulaji wa nguvu” ni Ujenzi. Kwahiyo, watu hao waliovutwa na Magufuli wachuma fedha nyingi katika nafasi zao. Kwa mfano, waziri mmoja mwandamizi enzi za Magufuli, alikabidhiwa jukumu la kununua “bombadia” za ATCL kwa fedha taslimu. Huyu jamaa alitengeneza mamilioni ya dola kama kamisheni kwenye ununuzi wa ndege hizo.
Na nguvu walizonazo Chato Gang ni moja ya sababu kuu ya kuhangaika kumhujumu Mama Samia kwani bila kuwa na mtu wa kuwalinda kama Magufuli, hawana amani na utajiri mkubwa waliochuma kupitia uswahiba wao na kiongozi huyo aliyefariki Machi mwaka huu.
Lakini pia utawala wa Magufuli ulipaswa kudumu milele. Tayari maandalizi yalikuwa yameanza kubadili katiba ili atawale milele. Na hili sio jambo lililotokea kwa bahati mbaya. Hapana. Ulikuwa mkakati uliopangwa muda mrefu ukishirikisha watu mbalimbali katika kada mbalimbali nchini Tanzania.
Hii ilikuwa himaya. Na Chato Gang wanahangaika kuirejesha himaya hiyo ambayo bila uwepo wa Magufuli, inaelekea kuanguka.
Kwa upande mwingine, anachofanya kiongozi huyo wa kidini na kisiasa ni dalili tu za tatizo lililodumu miaka kadhaa nchini Tanzania: UDINI. Makala hii haitoshi kueleza kwa kirefu kuhusu tatizo hilo lakini kwa kifupi, kila mara Tanzania inapokuwa chini ya rais Muislam, huwa kunaibuka “chokochoko” za kidini.
Utawala wa Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi ulikabiliwa na changamoto kubwa ya udini iliyotishia kusambaratisha amani na mshikamano wa Watanzania. Alipokuja Rais mstaafu marehemu Benjamin Mkapa, “chokochoko” hizo zilitulia, kabla ya kuibuka tena wakati wa utawala wa Rais mstaafu Jakaya Kikwete. Lakini Magufuli alipoingia madarakani, “chokochoko” hizo zilitulia tena.
Hata hivyo, ujio wa Mama Samia umeziibua tena “chokochoko” hizo. Na kwa kiasi kikubwa tu, vita ya Chato Gang dhidi ya Mama Samia ina chembechembe za udini pia.
“Adui” mwingine wa Mama Samia ni “uzanzibari” wake. Kama ilivyokuwa wakati wa utawala wa Rais mstaafu Mwinyi, kuliibuka harakati kubwa dhidi ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliozaa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni kipindi hicho ambako kuliibuka kundi maarufu la G-55 la wabunge wa Tanzania Bara waliotaka mabadiliko kwenye muundo wa muungano.
Kadhalika, ukweli kwamba Mama Samia ni mwanamke unawanyima baadhi ya wanasiasa waumini wa “mfumo dume” ambao hadi muda huu hawaamini kuwa nchi ipo chini ya Rais mwanamke.
Taarifa kuhusu kiongozi huyo wa dini na siasa zinaeleza kuwa kwa upande mmoja yeye na kundi lake wamefanikiwa kukiweka mkononi chama kimoja cha upinzani ambacho “kiliahidiwa na Magufuli kuwa kingepewa viti vya ubunge kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, na kukiwezesha kuwa chama kikuu cha upinzani.”
Vilevile, kundi hilo limefanikiwa kuwanasa baadhi ya viongozi wa chama kingine cha upinzani. Haikuwa nguvu kwa kundi hilo kufanikisha azma yao kutokana na “chuki iliyopo kati ya chama hicho na Mama Samia.”
Inaelezwa pia kuwa kundi hilo limejiweka karibu na wanaharakati walio karibu na chama hicho kwa minajili ya kutimiza ajenda hiyo.
Kesi dhidi ya Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Mheshimiwa Freeman Mbowe, imekuwa mtaji muhimu kwa kundi hilo, ambalo linaona kesi hiyo kama fursa adimu ya kuthibitisha kuwa “Mama Samia ni dikteta.” Kundi hilo linaamini kuwa kuna fursa ya kusambaza chuki zaidi dhidi ya kiongozi huyo.
Mwisho, kuna taarifa kuwa Idara ya Usalama wa taifa nayo imekuwa sehemu muhimu katika hujuma hizo, na inadaiwa kuwa “Mama Samia alihudhuria vikao vya CCM huko Dodoma hivi majuzi kwa kulazimisha, kinyume na ushauri wa Idara hiyo iliyomshauri asihudhurie.”
Katika hili, Mama Samia hana wa kumlaumu zaidi ya yeye mwenyewe kwani anaendelea kuwa “Rais wa ajabu” kurithi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa. Utamaduni usio rasmi katika nchi nyingi duniani ni kwa Rais mpya kuteua mkuu mpya wa Idara ya Usalama wa Taifa, kwa sababu huyo ndiye haswa “ameshikilia urais wa rais husika.”
Jumatano njema.