Shirika la Ndege la KLM la Uholanzi jana lilitangaza kusitisha baadhi ya safari zake kufuatia kilichoelezwa kuwa ni “uwepo wa tishio la kiusalama” jijini Dar es Salaam.
Wakati habari hizo zilipelekea shutuma kutoka kwa baadhi ya watu waliodai kuwa “hakuna tishio lolote Dar,” ripoti za kiintelijensia zinaeleza kuwa kuna uhusiano kati ya hatua hiyo ya KLM na tahadhari iliyotolewa juzi na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania.
Je matukio hayo mawili yana ukweli au ni hujuma tu kama wanavyodai baadhi ya wananchi nchini Tanzania?



