Safu ya MAISHA [Episode 5]: mfahamu Balozi Mbelwa Kairuki, balozi mpya wa Tanzania hapa Uingereza alikohamishiwa kutoka China ambako alifungua fursa mbalimbali kwa wafanyabiashara wa Kitanzania
Yayumkinika kuamini kuwa endapo itapigwa kura ya maoni ya kumpata “balozi Mtanzania mchapakazi kuliko wote” basi jina la Mheshimiwa Mbelwa Kairuki lazima litakuwepo kwenye tatu bora, na huenda akashika nafasi ya kwanza kabisa.
Balozi Kairuki amejibidiisha sana katika utendaji kazi wake tangu alipoteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini China mwaka .