Safu ya #HabariZaZanzibar: CCM ina mpango wa "kukopi mbinu ya Magufuli" ya kununua wapinzani kwa ajili ya uchaguzi mkuu 2025, ACT-Wazalendo yatahadharishwa
Japo si jambo geni kwa wanasiasa kuhama vyama, kilichojiri wakati wa utawala wa marehemu John Magufuli ambapo lundo la wanasiasa wa upinzani walihama vyama vyao na kujiunga na CCM, kitabaki kwenye kumbukumbu za historia ya Tanzania.
Kinachosikitisha zaidi ni kwamba hadi makala hii inaandikwa, si vyama vya upinzani vilivyoathiriwa na “hama hama” hiyo wala…