Rwanda: Rais Kagame afanya mabadiliko makubwa ya wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, ateua bosi mpya wa ushushushu wa ndani
Kigali, Rwanda, Juni 5,2023: Rais Paul Kagame wa Rwanda, ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa nchi hiyo, amefanya mabadiliko makubwa katika ngazi mbalimbali za juu za vyombo vya dola na usalama.
Katika mabadiliko hayo yaliyotangazwa jana, baadhi ya nafasi zilizoguswa na mabadiliko hayo ni pamoja na kuteuliwa kwa mkuu mpya wa ushushushu wa ndani wa Idara ya Usalama wa Taifa ya Rwanda inayofahamika kama NISS.