Rwanda: huku kukiwa na tetesi za mapinduzi, Rais Kagame awatimua jeshini zaidi ya wanajeshi 200 ikiwa ni pamoja na mkuu wa zamani wa ushushushu nchini humo

Rais Paul Kagame amewatimua zaidi ya wanajeshi 200 kutoka jeshi la nchi hiyo, miongoni mwao wakiwa maafisa 14.
Hatua hiyo imekuja siku moja tu baada ya Rais Kagame kufanya mabadiliko makubwa katika taasisi za usalama na ulinzi nchini humo.
Rwanda: Rais Kagame afanya mabadiliko makubwa ya wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, ateua bosi mpya wa ushushushu wa ndani
·
Kigali, Rwanda, Juni 5,2023: Rais Paul Kagame wa Rwanda, ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa nchi hiyo, amefanya mabadiliko makubwa katika ngazi mbalimbali za juu za vyombo vya dola na usalama. Katika mabadiliko hayo yaliyotangazwa jana, baadhi ya nafasi zilizoguswa na mabadiliko hayo ni pamoja na kuteuliwa kwa mkuu mpya wa ushushushu wa ndani wa Idara ya Usalama wa Taifa ya Rwanda inayofahamika kama NISS.