Ripoti ya kiintelijensia: matishio ya ugaidi kwa Tanzania yanayochangiwa zaidi na uwepo wa Watanzania kwenye miundombinu ya kigaidi Somalia, Msumbiji na DRC
![](https://substackcdn.com/image/fetch/w_1456,c_limit,f_auto,q_auto:good,fl_progressive:steep/https%3A%2F%2Fsubstack-post-media.s3.amazonaws.com%2Fpublic%2Fimages%2F2e533103-94b6-460f-8ea9-5fcfce6838b1_800x369.png)
MUHTASARI
Uwepo kwa raia wa Tanzania kwenye makundi ya kigaidi, kuendelea kujiunga na makundi hayo, na ushahidi kutoka kwa kesi mahakamani, inaweza kupelekea hitimisho la uwepo wa tishio la ugaidi kwa Tanzania kutoka Msumbiji, Kongo na Somalia.
Watanzania waliopo kwenye vikundi vya kigaidi na mitandao inayowezesha Watanzania hao kusafiri hadi nchi zinazokabiliwa na mashambulizi ya kigaidi ni changamoto kubwa kwa mamlaka za mitaa, serikali za kitaifa, na mataifa ya kigeni kote Afrika Mashariki.
Wakati mapambano dhidi ya ugaidi yameongezeka kwa umuhimu kwa serikali ya Tanzania na nchi hiyo ikichukua jukumu kubwa katika kukabiliana na tishio hilo, wingi wa raia wa Tanzania na mitandao inayojihusisha na makundi ya kigaidi ndani na nje ya nchi kunahitaji Idara ya Usalama wa Taifa ya Tanzania na mamlaka nyingine za ulinzi na usalama kujibidiisha kukabiliana na tishio hilo.