Ripoti ya kiintelijensia kuhusu tahadhari iliyolewa jana na Ubalozi wa Marekani kuhusu tishio la ugaidi Tanzania
Jana, Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ulitoa tahadhari ya kiusalama kuhusu uwezekano wa shambulizi la kigaidi.
Taarifa kamili kwenye tovuti ya ubalozi huu ni hii (kijarida hiki kimeitafsiri taarifa hiyo kwa Kiswahili)
Tahadhari ya Usalama - Ubalozi wa Marekani, Dar es Salaam, Tanzania
Mahali: Maeneo yenye msongamano mkubwa wa magari yanayotembelewa na watu wa Magharibi jijini Dar es Salaam na kwingineko nchini Tanzania
Tukio: Maeneo yanayotembelewa na raia wa Marekani na watu wengine wa [nchi za] Magharibi jijini Dar es Salaam na kwingineko nchini Tanzania yanaendelea kuwa shabaha za kuvutia kwa magaidi wanaopanga kufanya mashambulizi. Vikundi vya kigaidi vinaweza kushambulia bila onyo kidogo au bila onyo, wakilenga hoteli, balozi, mikahawa, maduka makubwa na soko, vituo vya polisi, misikiti na maeneo mengine yanayotembelewa na watu wa [nchi za] Magharibi.
Hatua za Kuchukua:
Kuwa macho kwa mazingira yako.
Fanya hatua za usalama wa kibinafsi.
Kaa macho katika maeneo yanayotembelewa na watalii/Wakazi wa [nchi za] Magharibi.
Weka wasifu wa chini.
Tembelea tovuti yetu kwa Kusafiri kwa Maeneo Ya Hatari Zaidi .
S. raia wanaosafiri nje ya nchi wanapaswa kuwa na mpango wa dharura kila wakati kwa hali za dharura. Kagua Orodha ya Hakiki ya Wasafiri .
Kwa kiasi kikubwa taarifa hiyo imepokelewa kwa hasira na makundi mbalimbali.
Kwa baadhi ya wafuasi wa Chadema, taarifa hiyo ya Ubalozi wa Marekani “haikugongana na ujio wa Tundu Lissu kwa bahati mbaya.” Kwao, taarifa hiyo ni ushirikiano kati ya Wamarekani na CCM kupata kisingizio cha kuzuwia mikutano.
Kwa wengine, taarifa hiyo imewakumbusha utawala wa marehemu Magufuli. “Ndio maana Magufuli hakupenda upumbavu wa aina hii,” alitamka kwa hasira kada mmoja wa CCM.
Miongoni mwa wana-CCM, taarifa hiyo ni “hujuma za mabeberu dhidi ya uchumi wa Tanzania.” Kada mmoja aliongea kwa uhakika mkubwa kwamba “hakuna cha ugaidi wala nini, hawa wanataka kuwatisha watalii.”
Lakini pia kuna “kundi la kawaida” lisilowapenda Wamarekani. Mkazi mmoja wa Kenya alidai “Wamarekani wanajifanya wajuaji sana, utadhani huko kwao ni salama.”
Ni watu wachache kabisa walioichukulia taarifa hiyo kwa uzito stahili.
Taarifa ifuatayo ya kiintelijensia inaeleza kwanini tahadhari hiyo iliyotolewa na ubalozi wa Marekani sio tu ni ya kweli bali pia inayopaswa kuchukuliwa kwa uzito mkubwa