Ripoti ya kiintelijensia kuhusu sababu iliyopelekea mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri hapo jana wakati mabadiliko mengine yapo njiani
Jana April 1, 2023, Rais Samia Suluhu alifanya mabadiliko madogo kwenye kabineti yake.
Japo mabadiliko hayo yalipotangazwa hayakuonekana kugusa hisia za watu wengi, kuna baadhi waliohoji “kulikoni” hasa ikizingatiwa kuwa mawaziri husika hawajakaa muda wa kutosha kwenye wizara husika.
Ripoti hii ya kiintelijensia inatanabaisha kuwa mabadiliko hayo yametokana na sababu moja ambayo hata hivyo ina uwezekano wa kupelekea mabadiliko mengine huko mbeleni.
Kadhalika ripoti inaelekeza kuhusu mabadiliko mengine ya kabineti ya Rais Samia ambayo “yapo njiani”.