Utangulizi: kwa siku kadhaa sasa, zimeenea taarifa katika mitandao ya kijamii kuhusu wapi alipo Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango. Lakini baadhi ya taarifa hizo za mtandaoni zilikwenda mbali hadi kudai kuwa kiongozi huyo wa pili kwa ukuu kitaifa “ametangulia mbele za haki”.
Taarifa zilizosambaa ni pamoja na:
Dokta Mpango yupo nje ya nchi kikazi.
Dokta Mpango anaumwa na yupo nje kimatibabu lakini hali yake si mbaya.
Dokta Mpango anaumwa na yupo nje kimatibabu na hali yake ni mahututi.
Dokta Mpango “ametangulia mbele za haki”.
Ripoti hii inatoa jibu kamili