Barua Ya Chahali

Share this post
Ombi Langu Maalum Kwako: Naomba Uungane Nami Kuadhimisha Siku Yangu ya Kuzaliwa Hapo Desemba 9 kwa Kumpa Tabasamu Mtoto Huyu Mwenye Ulemavu, Zakaria. Let's Do This!
www.baruayachahali.com

Ombi Langu Maalum Kwako: Naomba Uungane Nami Kuadhimisha Siku Yangu ya Kuzaliwa Hapo Desemba 9 kwa Kumpa Tabasamu Mtoto Huyu Mwenye Ulemavu, Zakaria. Let's Do This!

Evarist Chahali
Nov 28, 2021
Share this post
Ombi Langu Maalum Kwako: Naomba Uungane Nami Kuadhimisha Siku Yangu ya Kuzaliwa Hapo Desemba 9 kwa Kumpa Tabasamu Mtoto Huyu Mwenye Ulemavu, Zakaria. Let's Do This!
www.baruayachahali.com

Desemba 9 ni maadhimisho ya siku yangu ya kuzaliwa, siku ambayo pia ni birthday ya Tanganyika. Mara nyingi huwa naadimisha siku yangu ya kuzaliwa kwa kufanya tukio, aidh kuzindua kitabu au kitu kingine muhimu kwa jamii. Kwa sababu, uwepo wetu hapa duniani una maana tu endapo una maana pia kwa jamii.

Miongoni mwa mambo ninayopanga kuyafanya katika maadhimisho ya siku yangu ya kuzaliwa hapo Desemba 9 ni kumpatia tabasamu Zakaria, mtoto mwenye ulemavu ambaye yupo Msisi huko Dodoma.

Nilikutana na picha ya Zakaria huko mtandaoni. Nikauliza endapo kuna mtu anafahamu taarifa zake.

Twitter avatar for @ChahaliJasusi @Chahali
#MsaadaTutani: bado natafuta taarifa kuhusu mtoto huyu. Tafadhali nisaidie kusambaza ujumbe huu hadi uwafikie wazazi/walezi/walimu wake. Mungu awabariki sana
Image

July 31st 2021

78 Retweets176 Likes

Jambo la kusikitisha si kwamba tu upatikaji wa taarifa umekuwa mgumu lakini pia mwitikio wa wadau nao umekuwa haba. Hata hivyo, nilifanikiwa kupata mawasiliano na mdau mmoja ambaye anamfahamu mtoto huyo na changamoto anazozipitia kutokana na ulemavu. Nikadhamiria kufanya kila lilo ndani ya uwezo wangu kumsaidia.

Then wakati natafakari jinsi ya kuadhimisha siku yangu ya kuzaliwa nikaonelea hakuna namna mwafaka zaidi ya kusherehekea na Zakaria kwa kumpa tabasamu la kudumu. Juzi nika-post huko insta, na mapekeo yalikuwa mazuri, ambapo wadau mbalimbali walijitokeza na kuahidi kuungana nami kumpa tabasamu Zakaria.

Kwa upande wangu, mchango wangu kwa Zakaria ni kumhudumia mpaka nitakapoitwa mbele za haki. Bahati nzuri, kuna wadau watano kutoka Arusha japo wanafanya shughuli za Dar, nao wameahidi kutoa mchango endelevu kwa Zakaria.

Kwahiyo naomba kutumia Jumapili hii ya mwisho kwa mwezi huu wa Novemba kukuomba ujumuike nami kumpatia Zakaria tabasamu la kudumu. Pengine utajisikia kuni-wish happy birthday. Nitashukuru endapo “happy birthday” hiyo itakuwa kwenye kumpa tabasamu Zakaria.

Zoezi zima la Zakaria kukabidhiwa michango yake litarekodiwa na kila aliyechagia ataona kuwa mchango wake haujatafunwa na Jasusi.

Mdau anaye-coordinate zoezi hili huko nyumbani ni Ndugu Emmanuel Alfred Kundi. Unaweza kuwasiliana nae kwa namba 0719170081 ambayo pia ni namba ya TigoPesa.

Twitter avatar for @ChahaliJasusi @Chahali
Anaye-coordinate misaada kwa malaika huyo ni Mr EMMANUEL KUNDI, namba yake ya simu ni 0719170081 (ambayo pia ni namba ya TigoPesa). Ninai-dedicate birthday yangu hapo Desemba 9 kwa malaika huyu pamoja na kumgharamia kila kitu mpaka nitapoitwa mbele za haki.

November 26th 2021

2 Retweets21 Likes

Unaweza kuchangia chochote, si lazima fedha. Na kila kitakachochangiwa kitafikishwa kwa Zakaria.

Let’s do this guys!

Share this post
Ombi Langu Maalum Kwako: Naomba Uungane Nami Kuadhimisha Siku Yangu ya Kuzaliwa Hapo Desemba 9 kwa Kumpa Tabasamu Mtoto Huyu Mwenye Ulemavu, Zakaria. Let's Do This!
www.baruayachahali.com
TopNewCommunity

No posts

Ready for more?

© 2022 Evarist Chahali
Privacy ∙ Terms ∙ Collection notice
Publish on Substack Get the app
Substack is the home for great writing