Ndugu Zangu Madaktari Mmewasaliti Watanzania, Lakini Nao Wamejisaliti Pia

Image

Jana nilikutana na tamko la chama cha madaktari Tanzania (MAT) iliyokuwa inafanya siasa kwenye janga la UVIKO-19 (Ugonjwa wa Virusi vya Korona vya mwaka 2019) badala ya kuzingatia utaalam.

Baadaye nikakutana na bango hili

Image

Hawa ndugu zangu ni wahuni. Kwa sababu wanafahamu fika kilichotokea, kinachotokea na kijacho lakini wameamua kuthamini matumbo yao badala ya taaluma yao tukufu na uhai wa Watanzania. Watambue tu kuwa kila uhai wa Mtanzania unaopotea kutokana na hadaa hizi, nao pia wana damu ya marehemu kwenye mikono yao.

Hawa jamaa laiti wangeamua kuwa “liwalo na liwe,” na wakasimama na wanyonge wa Kitanzania wasio na wasemaji, basi jitihada za Serikali ya Magufuli kufanya hadaa kwenye janga hili isingefanikiwa.

Awali nilipata matumaini kidogo baada ya kuona wimbi la madaktari likivamia mitandao ya kijamii wakati janga la UVIKO-19 lilipoanza kupamba moto. Kwa vile nilishajua kuwa serikali ya Magufuli ingeficha ukweli kuhusu korona, nikatarajia madaktari hawa wangetusaidia kufahamu ukweli, si kwa kuhatarisha usalama wao kwa wao kutoa taarifa mitandaoni bali “kuzivujisha” kwa sie tulioamua kitambo “liwalo na liwe lakini ukweli lazima uwekwe hadharani.”

Lakini kadri siku zilivyokwenda huku Serikali ya Magufuli ikionyesha bayana kuwa inapuuza janga hilo, ukimya wa madaktari wetu uliashiria kuwa nao wameamua “kuunga mkono” jitihada za kuchezea uhai wa Watanzania katika janga hilo la UVIKO-19.

Sio kwamba tunalazimisha habari mbaya bali tunahitaji kuona Watanzania wanaambiwa ukweli badala ya kuhadaiwa. Kilichopo huko ni mkakati hatari wa Magufuli wa HERD IMMUNITY

Image

mbao kwa lugha nyepesi ni “mfe nyie wanyonge ili wasalimike wao wenye umuhimu kwa taifa.”

Kwa upande mwingine, kinachofanywa na madaktari wetu ni mwendelezo tu wan kinachofanywa na Watanzania wenyewe. Katika vipimo vyote vya udhaifu wa Watanzania, hili la korona litabaki kuwa nambari wani. How on earth watu milioni 59 wanaweza kumruhusu mtu mmoja azifanyie mzaha afya zao? Hivi watu walioridhia afya zao kufanyiwa mzaha wanawezaje kudai Tume Huru ya Uchaguzi au Katiba mpya?

Natumaini mtakumbuka angalizo hili: unless korona “igome kuondoka,” lakini mafanikio ya Magufuli katika mzaha huu anaowafanyia utampa jeuri isiyomithilika kwa sababu licha ya kuwachezea miaka mitano mfululizo bado mmempa ruhusa kubwa zaidi ya yote ya kufanya kamari kwenye uhai wenu.

Na pengine ni katika hali hii ndio maana hata hao madaktari hawakuona umuhimu wa kuhatarisha ajira zao kuwatetea watu wasiojielewa ambao kitu pekee kinachowahangaisha ni UBUYU.

Aliyewaroga Watanzania kapatwa na korona, kawekwa karantini, katoroka, kagongwa na kiberenge, kafariki. Hamponi!

Siku njema.

TANGAZO: Ninatarajia kufanya usajili mpya wa watu wanaotumiwa kijarida. Lengo ni kuwaondoa MATAGA waliojazana hapa.