[#TumiaVPN Endapo Link Haifunguki]Mzaha wa Magufuli Kwenye Korona: Yajayo Yanatafakarisha.

GADO - Coronavirus and Events in Tanzania | The Elephant

Mtu mmoja alinitwiti majuzi akidai “siaminiki” kwa sababu “nilibashiri korona itamwondoa Magufuli” lakini kwa mujibu ya mtu huyo “si kweli.”

Mtu huyu alikuwa anaongelea ubashiri niliofanya kwenye “Uchambuzi wa Kiintelijensia Kuhusu Mustakabali wa Urais wa Magufuli Kutokana na Jinsi Alivyoshughulikia Janga la Korona.”

Bado ninasimamia nilichokiandika katika uchambuzi huo wa kiintelijensia. Na sio kama ninakisimamia kwa vile tu nilikiandika mwenyewe au kwa kuchelea “kuiweka matatani heshima yangu kwenye jamii (kama ipo😊) bali kwa sababu uchambuzi huo haukutamka mahala popote kuwa urais wa Magufuli ungeisha siku au wiki kadhaa baada ya kuuchapisha.

Na licha ya kutahadharisha kuwa “intelijensia sio sayansi timilifu (intelligence is not exact science)” baadhi ya factors zilitegemea kutokea kwa factors nyingine. Kwa mfano, ubashiri kuwa baadhi ya “wapambe wa Magufuli” wangemgeuka ENDAPO idadi ya vifo kutokana na korona ingezidi kuongezeka, haujawa hivyo si kwa sababu idadi ya vifo vya korona haikuwa kubwa bali Magufuli amefanikiwa - angalau hadi muda huu - kuficha ukweli kuhusu janga hilo, kama alivyofanikiwa kuficha ukweli kuhusu idadi ya waliouawa na “kikosikazi” huko MKIRU (Mkuranga, Kibiti na Rufiji.

Na katika hilo la MKIRU, ninajisikia faraja kuwa Mtanzania pekee aliyejaribu kulitafutia ufumbuzi kwenye taasisi za kimataifa, kwa kuanzisha petition mtandaoni na “kupotea” kwa mwanahabari Azory Gwanda aliyekuwa akifuatilia suala hilo

Na japo nilikumbana na kikwazo, ukweli unabaki kuwa sio tu nilijaribu bali historia itanikumbuka kama Mtanzania pekee kufanya jitihada hiyo kimataifa.

Turejee kwa Magufuli. Japo amefanikiwa katika hilo la kuficha idadi ya vifo vya korona, si kwa sababu yupo smati kwenye kuficha taarifa bali tuna Wapinzani “wanaoshikilia bango yale tu wanayoona yana umuhimu kwao kisiasa,” sambamba na Watanzania wanaodanganyika kirahisi kama ilivyokuwa kwenye ishu za Babu Ambi

Au ‘Dakta’ Shika

Ndio ukweli huo. Ni rahisi kuwalaumu wanasiasa wa Upinzani kwa kutoMbana Magufuli ipasavyo kwenye ishu kama ya MKIRU au hiyo ya Korona lakini ni muhumi kukumbuka kuwa wanasiasa hao -kama wale wa CCM - ni kielelezo cha jinsi Watanzania walivyo. Kasoro zilizopo kwenye familia, kabila, ukoo baadaye huishia kuwa kasoro KITAIFA.

Nirejee kwenye uchambuzi wangu wa kiintelijensia kuhusu mustakabali wa urais wa Magufuli. Nilitanabaisha kuwa anguko lake linaweza kutokana na factors za KIUCHUMI, ndani na nje. Bila haja ya kurudia nilichaondika, uchumi wa nchi hutegemea both soko la ndani na la nje. Na masoko hayo mawili yanahusiana kwa karibu.

Moja ya mifano hai ni huu

Na kwenye soko la kimataifa, inaweza kuwa vigumu kwa mnunuzi anayetaka kununua bidhaa kutoka Tanzania kufanya hivyo baada ya kukutana na takwimu zisizopendeza kama hizi

Na licha ya athari za korona kwa utalii kwa takriban kila nchi, kwa Tanzania athari hizo zachangiwa na hiyo hatua ya Magufuli kuficha takwimu za korona

Naomba ieleweke kuwa kubashiri kuwa mustakabali wa urais wa Magufuli ni tete - na hata KUTAMANI aondoke madarakani - haimaanishi kuichukia Tanzania. Tofauti na mzaha wa MATAGA wa kumfanya “Magufuli ndio Tanzania,” au “hakuna Tanzania bila Magufuli,” ukweli ni kwamba Tanzania ilikuwepo, ipo na itaendelea kuwepo hata kama Magufuli asingekuwepo. Uhuru ulitafutwa na akina Nyerere, si Magufuli. Na hata huko kuifikisha Tanzania kwenye uchumi wa kati, ni jitihada za Watanzania kwa ujumla na si za mtu mmoja.

Nihitimishe makala hii kwa taarifa kuhusu jarida jipya la UJASUSI.

Ndimi mtumishi wako,

Evarist Chahali