Musiba ni MBWA tu. Mwenye MBWA huyo ni Magufuli

Vyovyote Itakavyokuwa, Mwisho Wao Wote Wawil Hautokuwa Mzuri

Natumiani nyote mlikuwa na Pasaka njema. Sikuwatumia #BaruaYaChahali jana kwa sababu ilikuwa Jumatatu ya Pasaka na sikutaka kuwasumbua.

Leo tunatupia jicho tena masuala ya siasa, japo kama nilivyoeleza katika matoleo mawili yaliyopita, nitaendelea kuwaletea mada nyingine licha ya siasa kila itapobidi.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, kama kawaida yake ‘toilet paper’ ya Musiba (gazeti la Tanzanite) iliendelea na misson yake ya kuchafua watu mbalimbali inaowaona kuwa ni wakosoaji dhidi ya Magufuli.

Safari hii mhanga wa Musiba alikuwa kijana mmoja mwanaharakati ambaye amekuwa mstari wa mbele kukemea maovu mbalimbali katika jamii. Katika namna inayoweza kufanywa na shetani tu, Musiba akadai kuwa kijana huyo ni shoga. Lakini kana kwamba hilo sio baya, shetani huyo akaenda mbali zaidi na kudai kuwa kijana huyo anasababisha ‘ugomvi’ kati ya wanasiasa wawili maarufu, akimaanisha kuwa wana mahusiano ya kishoga na kijana huyo.

Mie mtumishi wako nimekuwa mhanga wa kawaida wa Musiba. Hata hivyo, kwa upande wangu, kuna mtu maalum huko Ikulu anaitwa Jeswald Majuva ambaye ndiye anashughulikia “habari chafu” dhidi yangu kwenye magazeti ya Musiba.

Image result for JESWALD MAJUVA

Huyu bwana ni mtu wa kitengo ambaye pia ni mmoja wa wasaidizi wa karibu wa Magufuli.

Na uhusika wa Majuva kwenye gazeti hilo unasaidia kuthibitisha madai yaliyotolewa majuzi na Zitto Kabwe kuwa ‘toilet papers’ za Musiba huchapishwa na kiwanda cha uchapaji cha Idara ya Usalama wa Taifa (Malindi Printing Press) kilichopo Malindi, Mbweni, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, kwenye chuo cha Idara hiyo.

Lakini pengine kinachokera zaidi kuhusu suala hili ni unafiki wa Magufuli. Wakati flani baada ya moja ya magazeti ya Musiba kumchafua mtu flani, Magufuli alimpigia simu ndugu ya karibu wa mtu huyo aliyechafuliwa akidai kusikitishwa na kitendo cha gazeti hilo. Yaani kwa lugha nyingine, alikuwa anajaribu kukwepa lawama za uhusika wake katika mpango huu wa kishetani wa kuwachafua watu.

Kwahiyo, japo ni sahihi kuchukizwa na ushetani wa Musiba, ni muhimu kutambua kuwa yeye ni mbwa tu, ilhali mwenye mbwa ni Magufuli. Ni Magufuli anayeidhinisha fungu la zaidi ya Shilingi milioni 100 kwa magazeti ya Musiba ili yaendelee kutuchafua.

Waweza kusema “ah kwani mie inanihusu nini?” Wewe hutokuwa wa kwanza kujidanganya hivyo. Mara ya kwanza kabisa Musiba kujitokeza hadharani ni pale alipotutangaza watu tisa kuwa ni #WatuHatari. Licha ya watu kadhaa kukerwa na kitendo hicho, idadi kubwa ya watu sio tu waliona ni suala la kawaida tu bali pia waliamini kuwa suala hilo haliwahusu.

Mwaka mmoja baadaye, Musiba amewaandama mamia ya watu ikiwa ni pamoja na waliochukulia suala la #WatuHatari kuwa haliwahusu.

Pengine unaweza kujidanganya kuwa “mie ni nani hasa hadi niandikwe na Musiba?” Well, sio lazima akuandike bali ni muhimu utambue kuwa kama Rais wako anaweza kumtumia Musiba kuwachafua watu wasio na hatia, atashindwa nini kukuhujumu wewe “mtu wa kawaida”?

Jana usiku nilitumiwa clip moja ya Musiba akiendeleza mashambulizi dhidi ya huyo kijana mwanaharakati. Katika clip hiyo, shetani huyo anamtukana kijana huyo mara kadhaa. Pia anaagiza Magufuli amkamate kijana huyo kisha alawitiwe “kwa sababu ni shoga.” Kana kwamba kutaka mtu asiye na hatia alawitiwe sio jambo baya, bado shetani huyo anamwandama kijana huyo kuwa ni shoga.

Naweza kuandika kutwa nzima kuhus ishu hii ambayo nami ni mhanga wa mara kwa mara lakini la muhimu sio kuendelea kulalamika pasi kuchukua hatua stahili. Kunahitajika hatua za muda mfupi na hatua za muda mrefu. Hatua za muda mfupi ni kama hizi nilizobainisha kwenye tweet yangu ya hivi karibuni

Hatua za muda dhidi ya Mbwa huyu ni kumkabili mwenye mbwa. Kwa sababu hata Musiba akishughulikiwa bado Magufuli atamtumia Musiba mwingine. Ieleweke kuwa Musiba hafanyi haya kwa sababu anamchukia Chahali au Zitto Kabwe au Maria Sarungi. Hapana. Musiba anatumwa na Magufuli. Kwahiyo adui hasa wa wahanga wa Musiba ni Magufuli. Kwa maana hiyo, baada ya hatua za muda mfupi kumshughulikia Musiba ni lazima kuwepo hatua za muda mrefu kumshughulikia mwenye mbwa yaani Magufuli.

Nihitimishe barua hii kwa kutanabaisha kuwa mwisho wa haya yote upo njiani, na ukiwadia, nyote mtakuwa mashahidi. Ni rahisi kwa Magufuli na mbwa wake kudhani atatukandamiza muda wote. Ni rahisi pia kudhani atakandamiza watu wote. Lakini kwa hakika hawezi kutukandamiza watu wote kwa muda wote. Kila jambo lina mwisho wake, hata kama mwisho huo utachukua muda mrefu kufikiwa.

Nakutakia siku na wiki njema.Tukutane wiki ijayo panapo majaliwa.

Mtumishi wako

Evarist Chahali