Mtume Aliyesababisha Vifo 20 Hakukamatwa. Kwanini Serikali ya Magufuli Inawaongopea Kuwa Alikamatwa Na Sasa Kapewa Dhamana?

Nchi Inaendeshwa Kama Kampuni ya Genge la Kihalifu

Tangu mwanzo wa tukio la vifo 20 (bado naambiwa kuwa idadi ya waliofariki ni kubwa zaidi) hisia yangu ya sita ilikuwa inaniambia “hapo kuna namna.”

Kwenye ushushushu inasisitizwa kutoamini COINCIDENCE (matukio mawili au zaidi yanayotokea kwa wakati mmoja au mfululizo). Ukweli kwamba tukio la vifo hivyo huko Moshi lilijiri masaa machache tu baada ya Marekani kutangaza kuwa imempiga marufuku Bashite kukanyaga nchi hiyo, ulinifanya “nichezwe na machale.”

Anyway, kwa kifupi, taarifa kwamba “Mtume” aliyehusika na vifo ameachiwa kwa dhamana ni za UONGO.

Ni uongo kwa sababu mtu hawezi kuachiwa kwa dhamana kama hakukamatwa in the first place. Naam, “Mtume” aliyesababisha vifo hivyo 20 sio tu hakukamatwa lakini bali pia amri ya kutomkamata ilikuwa “maagizo kutoka ngazi za juu.” Na ndio maana hakuna picha ah video inayomuonyesha “Mtume” huyo akiwa mikononi mwa polisi.

Lakini hata tukiweka kando suala la picha, taarifa ya Waziri Simbachawene kuwa polisi walikuwa wamemkamata “Mtume”

sio tu ilikuwa urongo maana “Mtume” aliendesha ibada kama kawaida,

bali pia IGP Sirro alidai wanamtafuta “Mtume” huyo.

Haihitaji uelewa wa utendaji kazi was polisi kubaini kuwa mtu akikamatwa na polisi hawezi kutafutwa na polisi.

Kwanini “Mtume” huyo anakingiwa kifua?

Pamoja na sababu nyingine, kuu ni kwamba “Mtume” huyo ni “mtu wa Kamati ya Ufundi” ya Jiwe na mwanae.

Nadhani wengi wenu mnafahamu kuwa baadhi ya haya makanisa mapya yanatumia “nguvu za giza.”

Na “wambeya” wanadai kuwa hata hivyo vifo 20 ni “kafara ya baba na mwanae baada ya upepo wa kisulisuli kuvuma kutoka Marekani.”

Jiwe kwa mara ya kwanza amegundua kuwa “anawindwa na mabeberu,” na anajua bayana kuwa mabeberu hao wakiamua kwa dhati asirudi Ikulu hapo Oktoba, HATORUDI.

Lakini hata kama “Mtume” angekuwa amekamatwa kweli, kwanini aachiwe kwa dhamana ilhali anakabiliwa na kosa kubwa zaidi ya akina Eric Kabendera ah Tito Magoti wanaonyimwa dhamana kila kukicha ilhali makosa tao ni ya kutungwa tu?

Nimalizie kwa kuwakumbusha kuwa Tanzania ya Magufuli inaendeshwa kama kampuni ya genge la Mafia. Kuna uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu. Kuna dharau kubwa dhidi ya Katiba. Kuna jeuri dhidi ya hisia zenu walalahoi, kwamba hata mkifanywa nini hamna jeuri ya “kulianzisha.”

Nimalizie pia kwa kubashiri kutokea kwa tukio jingine kubwa katika wiki hii. Sintoshangaa kusikia Membe amevuliwa uanachama, au “breaking news “ kama hizo.

Ndimi jasusi wako,

Evarist Chahali