Mnaoshangilia anguko la Kamala kwa sababu ya "uswahiba wake na Mama Samia" aidha hamumjui Trump vizuri au mnajihadaa makusudi
Kabla ya yote Jasusi anawaomba radhi kwa ubashiri wake kwamba Kamala Harris angeshinda urais wa Marekani kwenda fyongo. Waungwana wakikosea huomba msamaha badala ya kukimbilia kutoa visingizio, au kuhalalisha makosa yao.
Jasusi anawashukuru mamia - pengine maelfu - mliomsihi afanya ubashiri huo kwa sababu moja kuu: imani yenu kwake. Na japo hakuwa na uha…