Barua Ya Chahali

Share this post
Mkuu Mpya Wa Idara Ya Usalama Wa Taifa, Diwani Rajabu, Amefeli Vibaya 'Mtihani Wa Kwanza'
www.baruayachahali.com

Mkuu Mpya Wa Idara Ya Usalama Wa Taifa, Diwani Rajabu, Amefeli Vibaya 'Mtihani Wa Kwanza'

Evarist Chahali
Jan 28, 2020
17
Share this post
Mkuu Mpya Wa Idara Ya Usalama Wa Taifa, Diwani Rajabu, Amefeli Vibaya 'Mtihani Wa Kwanza'
www.baruayachahali.com
Tanzania’s head of intelligence service Diwani Athuman Msuya swears in

Twiti hii hapa chini niliandika mie mtumishi wako mara baada ya kushiriki kikamilifu kumpigia kampeni mgombea wa CCM kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, John Magufuli

Twitter avatar for @ChahaliEvarist Chahali @Chahali
.@MagufuliJP you're a blessing, reincarnated Nyerere+Sokione in one, exceedingly patriotic, rare gem...Asante sana!
Image

November 23rd 2015

10 Retweets15 Likes

Na enzi hizo tulikuwa tunaona raha kuskia hotuba za mwanasiasa huyo. Na moja hotuba zilizonipa matumaini makubwa kuhusu Magufuli ni ile aliyoitoa siku ya ufunguzi wa “Bunge la Awamu ya Tano.”

Twitter avatar for @ChahaliEvarist Chahali @Chahali
.@MagufuliJP alipohutubia Bunge jana Novemba 20, 2015: Hapa ni video kamili ya hotuba hiyo ya kihistoria
Rais Magufuli ahutubia na kufungua bungeRais Magufuli ahutubia na kufungua bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Novemba 20, 2015.youtu.be

November 21st 2015

7 Retweets6 Likes

Lakini haikuchukua muda mrefu kwa baadhi yetu kubaini kuwa “tuliingizwa mkenge.” Japo sijutii kumsapoti Magufuli kwenye kamepni zake za mwaka 2015, kwa sababukwa upande mmoja alikuwa ndio njia pekee ya kumzuwia Lowassa kuingia Ikulu, na kwa upande mwingine alionekana kama mwanasiasa aliyekuwa na dhamira ya dhati ya kuwatumikia wanyonge. How he fooled us is another story. And the rest is now history.

Kwahiyo mara baada ya kubaini kuwa Magufuli katuingiza mkenge baadhi yetu tuliotoka povu kumnadi, nikapoteza hamu ya kusikiliza porojo zake majukwaani. Lakini kilichonifanya nizichukie hotuba zake ni ukweli kwamba nyingi - kama sio zote zimesheheni mipasho, ubabe, udhalilishaji na kila baya unaloweza kufikiria.

Ndio maana hata jana niliposikia kuwa hafla ya kuapisha wateule wake, which meant uwepo wa hotuba, sikuwa na muda mbovu kusikiliza “vichambo.”

Twitter avatar for @ChahaliEvarist Chahali @Chahali
Kichambo coming near you shortly!

millardayo @millardayo

Kutoka Mwanza Aiport, Viongozi wa Serikali,kisiasa, kidini, Wasanii na Wananchi mbalimbali tayari wamejitokeza kwa ajili ya kuipokea Bombadier Q400, Ndege hiyo ilikuwa imezuiliwa Canada kutokana na madai ya Mkulima, Hermanus Steyn na tayari imeanza safari yake kuja Tanzania. https://t.co/st191yPckY

December 14th 2019

5 Likes
Twitter avatar for @ChahaliEvarist Chahali @Chahali
Kichambo coming near you live and direct from Zanzibar 😊

January 10th 2020

18 Likes

Lakini licha ya kutoisikia hotuba hiyo ya jana, nimebahatika kupata dondoo za baadhi ya aliyoyaongea. Na moja lililonigusa kiasi cha kupelekea kuandika makala hii ni hili

Jambo moja ambalo Magufuli hajalitamka - kwa sababu zilizo wazi - ni kwamba Mkurugenzi Mkuu “mpya” wa Idara ya Usalama wa Taifa, Diwani Rajabu, AMEMWANGUSHA. Kwa sababu, laiti DGIS Diwani na Idara yake ya Usalama wa Taifa ingewajibika ipasavyo, mkataba huo usingesainiwa in the first place.

Kwanini namtaja Diwani moja kwa moja? Kwa sababu tofauti na Wakurugenzi Wakuu waliopita wa Idara hiyo, ni yeye pekee ambaye kabla ya kushika wadhifa ho alikuwa afisa mwandamizi wa jeshi la polisi kabla ya baadaye kuja kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU. Ukichanganya na ukweli kuwa huyu bwana ni Afisa Usalama wa Taifa “tangia zamani hizo,” hana sababu ya yeye na Idara yake kushindwa kuzuwia ufisadi huo.

Pengine waweza kuona jambo hili ni dogo na hata ukahisi sio sahihi kumalumu DGIS Diwani na TISS yake. However, let this sink in: kama iliwezekana kwa maafisa waandamizi wa serikali kwenda nje ya nchi kusaini mkataba huo - katika zama hizi ambapo safari za watumishi wa umma sio tu huruhusiwa kwa kibalimaalum bali pia hufuatiliwa kwa karibu na “Kitengo” - inashindikanaje kwa MAGAIDI kuingia nchini na “kufanya vitu vyao”?

Au tuiweke katika scenario tofauti: what if hao watendaji wa umma wasingekwenda kusaini mkataba wa kifisadi bali kushughulikia mkakati wa kulihujumu taifa kiusalama?

Ukweli mchungu ni kwamba Idara yetu ya Usalama wa Taifa ipo ipo tu. Kitu pekee inachojitahidi vizuri ni kufuatilia “akina Chahali wameandika nini,” au “wanaharakati wanaongea na nani, wametwiti nini…” au kile mahiri kwenye ubora wao, yaani kuvihujumu vyama vya upinzani. Na sasa wamejipa jukumu la kufuatilia nyendo za kila mwana-CCM anayedhaniwa atapambana na Magufuli kwenye uchaguzi mkuu.

Wakabidhi matishio halisi ya usalama wa taifa letu, hawa wahuni ni weupe kabisa. Na kibaya zaidi, Magufuli naye kajaza watu wake hao wanaoitwa MATAGA ambao takriban wote hawajui kwanini ni waajiriwa katika taasisi hiyo muhimu.

Pengine unaweza kusema “ah sasa si Diwani na vijana wake ndio wamemshtua Rais…” Well, laiti wazembe hao wangekuwa wanajua wajibu wao ipasavyo, suala hilo lisingefika hapo lilipofikia. Nasema hivyo kwa sababu moja ya majukumu makuu ya Idara yoyote ile ya Usalama wa Taifa ni PRE-EMPYTING vitendo vya adui, yaani kuvizuwia kabla havijatokea. Sasa kama walikuja kumjulisha Rais baada ya watu kuwa wameshafanya vitu vyao, pata picha ingekuwa ni suala la ugaidi…

Najua bayana DGIS Diwani hatopendezwa na “lawama hizi” na ana uhuru wa kufanya hivyo lakini anaweza pia kuichukulia makala hii kama constructive criticism na kufanyia kazi mapungufu yaliyopo.

Mie kama mdau wa sekta ya usalama wa taifa sintochoka kuwaamsha hao wazembe huko kitengo kwa sababu jukumu la kuiweka Tanzania salama sio suala la hiari bali la lazima. Na ili Tanzania iwe salama “kweli kweli” ni lazima Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa na maafisa wake waache uzembe na kuchapa kazi “kweli kweli.”

Ndimi jasusi wako

Evarist Chahali

Comment
Share
Share this post
Mkuu Mpya Wa Idara Ya Usalama Wa Taifa, Diwani Rajabu, Amefeli Vibaya 'Mtihani Wa Kwanza'
www.baruayachahali.com

Create your profile

0 subscriptions will be displayed on your profile (edit)

Skip for now

Only paid subscribers can comment on this post

Already a paid subscriber? Sign in

Check your email

For your security, we need to re-authenticate you.

Click the link we sent to , or click here to sign in.

TopNewCommunity

No posts

Ready for more?

© 2022 Evarist Chahali
Privacy ∙ Terms ∙ Collection notice
Publish on Substack Get the app
Substack is the home for great writing