Asubuhi hii - kwa mida ya Uingereza - kulikuwa na mjadala mzito katika mtandao wa kijamii wa Clubhouse ambako kuna jukwaa maarufu la Watanzania linalofahamika Sauti ya Watanzania
Mjadala huo ulihusu jinsi ya harakati dhidi ya Samia Suluhu Hassan na utawala wake zinavyoendeshwa. Hoja iliyotawala ilikuwa kwamba watu wengi wamejikita kwenye maongezi zaidi, hasa kinachoitwa “nondo” (hoja nzito) kuliko vitendo.
Aliyepigia mstari zaidi hoja hiyo alikuwa mmoja wa wana-Sauti ya Watanzania maarufu zaidi, Dkt Willbrod Slaa, aliyesema kuwa japo nondo ni muhimu lakini ni muhimu zaidi watu wajikite kwenye vitendo zaidi.
Alitolea mfano taarifa za mkutano wa Chama cha. Wabunge Duniani (IPU) utakaofanyika mwezi ujao jijini Arusha, ambao alisema ni fursa adimu kuonyesha upinzani dhidi ya Samia na serikali yake.
Kadhalika, kwamba Makamu wa Rais Deo Ndejembi aliwasili Marekani na hatimaye kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa bila hata mtu mmoja kujitokeza angalau na bango moja, imeonekana kuwa ni mapungufu makubwa.
Kadhalika, ziara ya Bashite kwenye klabu ya Barcelona huko Uhispania ambayo imeenda bila vipingamizi, imeelezwa kuwa ni moja ya ishara ya kuendekeza nondo zaidi ya vitendo.
Kwa upande mwingine, clip ya rapa maarufu wa Marekani Rick Ross akimsifia Samia na Makonda lakini bila kujibiwa kikamilifu na watu wengi, pia imeelezwa kuwa ni mapungufu kwenye harakati dhidi ya SAMIA na serikali yake.
Je una maoni gani?


