Mgogoro NCCR-Mageuzi: Kada wa Chadema Martin Maranja adai "mradi wa kumuondoa Mbatia ni wa Zitto na dola". Amtuhumu Naibu Msajili Nyahoza kuwa anakamilisha kazi ya Zitto. Amhusisha pia Evarist Chahali
Kada wa Chadema Martin Maranja Masese ametoa tuhuma nzito dhidi ya Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, Mheshimiwa Zitto Kabwe kuhusiana na jaribio la mapinduzi dhidi ya Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Taifa, Mheshimiwa James Mbatia.
Katika bandiko lake kwenye ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter lililochapishwa jana Mei 22 mnamo saa 9 na dakika 55 kwa majira ya hapa Uingereza, kada huyo alidai kwamba, namnuku,
Mradi wa kumuondoa James Mbatia ni mradi wa Zitto Kabwe na dola. Tunajua jambo la Zitto ni lako (mimi Evarist Chahali) pia. Zitto aliwalipia wajumbe wa NCCR kwenda Dodoma kwenye TCD ili kumkomoa Mbatia aliyesusia. [Sisty] Nyahoza (Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa Tanzania) anakamilisha kazi ya Zitto. Chadema hatuna ugomvi na NCCR. Tunaitaka NCCR imara.

๐๐๐ฌ๐ฎ๐ฌ๐ข @Chahali
Naona kuna jitihada kubwa miongoni mwa baadhi ya wana-CDM kumnusuru Mbatia. Ushirikiano baina ya vyama ni jambo jema. However, Mbatia anavuna alichopanda. I guess wanaomsapoti wamesahau "mkataba baina ya Mbatia na Mwendazake" 2020, only that the latter took the former for a ride https://t.co/2Wnk3wH6YgKada huyo mwenye wafuasi 355,131 alitoa tuhuma hizo nzito alipojibu hii ya twiti yangu (Evarist Chahali)


Twiti hiyo yangu kama Evarist Chahali ilikuwa ikizungumzia twiti ya Meya wa zamani wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob aliyekuwa akieleza kuhusu mgogoro unaoendelea wa chama cha NCCR-Mageuzi
Twiti hiyo ya tuhuma za kada huyo ilipata ritwiti ya mwanaharakati maarufu mtandaoni Maria Sarungi mwenye wafuasi zaidi ya milioni moja (ikimaanisha kuwa imeonwa na watu wengi)
Hadi wakati makala hii inachapishwa, twiti hiyo ilikuwa na ritwiti 54 na โlikesโ 410.
Jitihada za kumpata Mheshimiwa Zitto kuongelea tuhuma hizo hazikuzaa matunda lakini mimi kama Evarist Chahali bado natafakari hatua stahili za kuchukua kutokana na uzito wa tuhuma hizo.
Tuhuma hizi zinakuja siku chache tu baada ya Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Mheshimiwa Freeman Mbowe, kuwakemea vikali vijana wa chama hicho na kuwataka wawe na heshima na staha hata kwa watu wanaotofautiana nao kifikra.


Kadhalika, Mheshimiwa Mbowe alisisitiza kuhusu heshima kwa viongozi wa vyama vingine
Wakati hayo yakitokea, kada huyo wa Chadema alimtuhumu Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya CCM, Mheshimiwa Neema Lugangira, kumtumia twiti ambazo kwa maelezo ya mbunge huyo ni twiti feki






Jitihada za kumpata Mheshimiwa Neema kusikia reaction yake kuhusiana na twiti hizo zinaendelea.
Makala hii ni endelevu
Siku na wiki njema.