'Meseji Za Tigo' Ambazo Kigogo Anadai Zitatumika Kama Ushahidi Dhidi Ya Mbowe Ni Meseji Feki Alizotengeneza Yeye Na Genge Lake Kuuhujumu Uongozi wa Chadema

Meseji ambazo Kigogo anadai afisa wa kampuni ya Tigo ataziwasilisha mahakamani kama ushahidi dhidi ya Mheshimiwa Freeman Mbowe ni meseji feki alizozitengeneza akishirikiana na watu kadhaa.

Kigogo ambaye jina lake halisi ni Didier Abdallah Mlawa na kwa sasa anaishi hapa Uingereza kama mkimbizi ameshirikiana na watu kadhaa katika mpango huo dhalimu. Miongoni mwa watu hao ni Afisa wa Idara ya Usalama wa Taifa - kifupi cha majina yake IZ - ambaye yupo hapa Uskochi kwa kipenyo kama Mfamasia. Mwingine ni mwanamke mmoja Mtanzania -kifupi cha majina MM- pia ambaye amekuwa akishirikiana na Kigogo tangu mwaka 2018. Mwanamke huyo amekuwa akitumika kwa namna kadhaa. Kwa upande mmoja ni yeye na “mpenzi wake wa kike,” mwanamke mmoja - vifupisho NS - mtoto wa kiongozi wa zamani wa kitaifa. Huyu licha ya kuwa kada mwandamizi wa CCM pia ni mtu wa Kitengo.

Kwa upande mwingine, mwanamke huyo MM anatumiwa na mbunge wa zamani wa Chadema ambaye sasa ni Mkuu wa Wilaya. MM aliwahi kumdeti mbunge huyo wa zamani alipokuwa hapa UK.

Kilichofanywa na Kigogo kwa kushirikiana na genge hilo ni kutengeneza mawasiliano feki yanayojenga picha feki pia kwamba viongozi kadhaa wa Chadema walikuwa na mpango wa kufanya vitendo vya ugaidi. Katika mkakati huo haramu, Kigogo anajifanya kuwa alihusishwa kwenye mkakati huo wa ugaidi.

Pamoja na sababu nyingine, Kigogo anataka “kuua ndege wawili kwa jiwe moja.” Kwa upande mmoja mkakati hu haramu utampa fursa ya kulipa kisasi kwa Chadema waliomtimua baada ya kuleta ushauri wake wa kijinga kukitama chama hicho kijihusishe na vitendo vya vurugu kufuatia kukamwatwa kwa Mbowe. Tangua Chadema wakatae ushauri huo, Kigogo amekuwa bize kwenye kampeni ya matusi na kashfa dhidi ya viongozi waandamizi wa chama hicho.

Kwa upande mwingine, Kigogo anataka kutumia suala hilo kumalizana na serikali kwa sababu bado ana kesi ya kukimbia kifungo cha miaka 15 jela ambacho alihukumiwa mwaka 2015

kufuatia wizi wa shilingi 177.3 za kampuni ya Scania jijini Dar mwaka 2013

Bonyeza HAPA kusoma habari kamili kuhusu ujambazi huo wa Kigogo, kutorokea Kenya na hatimaye kupata ukimbizi hapa UK.

Awali jasusi aliwatahadharisha Chadema kuwa Kigogo kuhusu mpango huo haramu

Je Chadema wafanyeje?

Kwa kutumia wanasheria wake, Chadema inaweza kumuingiza Kigogo kwenye kesi hiyo kwa sababu amekuwa akiongea upuuzi wake kama mtu mwenye ushahidi usio na shaka dhidi ya Mheshimiwa Mbowe.

Nihitimishe kwa kukumbushia tu kuwa Agosti mwaka jana nilitahadharisha kuhusu mkakati wa Kigogo dhidi ya Upinzani, lakini tahadhari hiyo ilipelekea mtu huyo kuahirisha mkakati huo.