Barua Ya Chahali

Share this post
Mchungaji Msigwa 'Aamuriwa' na Lema Kufuta Twiti Iliyoshauri Kuwa Chenge Ndio Anafaa Kuwa Spika, Aifuta, Kisha Airejesha 'Kiaina.'
www.baruayachahali.com

Mchungaji Msigwa 'Aamuriwa' na Lema Kufuta Twiti Iliyoshauri Kuwa Chenge Ndio Anafaa Kuwa Spika, Aifuta, Kisha Airejesha 'Kiaina.'

Evarist Chahali
Jan 11
1
Share this post
Mchungaji Msigwa 'Aamuriwa' na Lema Kufuta Twiti Iliyoshauri Kuwa Chenge Ndio Anafaa Kuwa Spika, Aifuta, Kisha Airejesha 'Kiaina.'
www.baruayachahali.com

Majuzi, Mbunge wa zamani wa jimbo la Iringa Mjini kwa tiketi ya Chadema, Mchungaji Peter Msigwa, “aliamuriwa” na kiongozi mwenzie wa chama hicho, Godbless Lema, Mbunge wa zamani wa jimbo la Arusha Mjini, kufuta twiti iliyoshauri kuwa mwanasiasa mkongwe wa CCM, Andrew Chenge, ndiye anafaa kuwa spika.

Hata hivyo, inaelekea twiti hiyo haikumpendeza Lema, na “akamwamuru” Msigwa aifute twiti hiyo.

Na Mchungaji Msigwa “akatii amri hiyo.”

Lakini siku moja baadaye, Mchungaji Msigwa akairejesha twiti hiyo “kiaina” ikiwa ni “screenshot” lakini haikuambatana na neno lolote lile.

Pengine sio ishu kubwa kihivyo hadi iandikiwe makala, lakini haina ubaya kuiweka kwenye kumbukumbu za matukio mbalimbali katika safari yetu ya kujenga demokrasia ya kweli.

Tukio hilo linaweza kuwa na tafsiri kadhaa, lakini moja ya wazi ni kwamba haikuwa sahihi kwa Lema “kuingilia uhuru wa Mchungaji Msigwa” tena hadharani.

Lakini kwa kusoma comments zilizoambatana na twiti husika, si ngumu kuelewa kwanini Lema alifanya hivyo. Ni kwamba kama ambavyo sie wengine tusio wana-Chadema tunavyoishia kutukanwa pindi tukiongea chochote ambacho wafuasi wa chama hicho hawaafikiani nacho, ndivyo inavyoelekea kuwa kwa viongozi na wafuasi wa chama hicho, kwamba “ni kosa la jinai kuongea mawazo yanayokinzana na wengine.”

Na nyingi ya comments alizorushiwa Mchungaji Msigwa zilionekana kuungana na mtazamo wa Lema “kubinya uhuru wa maoni” wa mwanasiasa mwenzake.

Tukio hilo limenikumbusha “janga” nililokumbana nalo jana huko Instagram, ambapo niliweka maoni yangu kwenye bandiko flani, nikionyesha mshangao kwanini Chadema haijachukua hatua za kisheria dhidi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa “kufoji barua ya Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika,” kuthibitisha majina ya wabunge 19 wa viti maalum.

Wakati Mnyika akisema hakuwasilisha jina lolote kwa Tume hiyo, Tume ilidai ina ushahidi wa barua kutoka kwa Mnyika ikiwa na majina ya akina Halima Mdee.

Kada mmoja wa kike alinivamia kama mbogo na kudai “Chadema wakashtaki Kenya au Tanzania?” Nikamuuliza kwani kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Taifa cha chama hicho ipo mahakama ya Kenya au Tanzania? (Nikimaanisha kwamba “kama una imani kwa mahakama kuendesha kesi dhidi yako, basi ni wazi utakuwa pia na imani kwa mahakama kuendesha kesi utakayofungua dhidi ya mtu mwingine. Simple logic). Kada husika akakimbilia matusi.

Kwa tunaosoma mienendo mbalimbali katika Tanzania yetu, yayumkinika kutanabaisha bila shaka kuwa Chadema inazidi kuwa “chama cha mrengo mkali” (extremist) kinyume na neno “demokrasia” lililomo kwenye jina la chama hicho, CHAma cha DEmokrasia na MAendeleo.

Kuna sababu kadhaa na mabadiliko hayo ya kimrengo. Moja ya wazi ni ukweli kwamba “mtu akionewa sana anaweza kuishia kuwa mwonevu pia.” Kwamba vitendo mfululizo vya ukandamizaji wa haki za kikatiba za viongozi na wafuasi wa chama hicho vinaweza kuwa vimewafanya baadhi kuona “uungwana hauna maana.”

Sababu nyingine ni “radical elements” kutoka nje ya chama hicho, hususan “wanaharakati wa mtandaoni.” Kwa hawa, “upole au uungwana wa wana-Chadema” si habari njema kwao. Ni wazi, kwa mfano, Chadema ikiridhia jitihada za awali zinazofanyika kuhusu mchakato wa Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi, kupitia Kikosi Kazi cha akina Zitto Kabwe, “wanaopiga hela” kwa alama za reli mtandaoni (hashtags) wataathirika.

Kadhalika, wafuasi wengi wa chama hicho mtandaoni ni “watu wasiojulikana”, kitu kinachowapa “jeuri ya kutukana ovyo” kwa sababu “hawajulikani.” Waasisi wa uhuni huu ni CCM ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakitumia akaunti feki kwenye mitandao ya kijamii kudhibiti maoni “wasioyapenda.” Wakati wa utawala wa Magufuli, uhuni huo ulichukua sura mpya kupitia vyombo rasmi vya habari vilivyomilikiwa na yule “jahili” Musiba (sijui ana hali gani baada ya kusikia Mama Samia “kawapa rungu” Ridhiwani Kikwete na Nape Nnauye, ambao Musiba aliwachafua mfululizo).

Nihitimishe kwa angalizo kuhusiana na kijarida hiki. Bila shaka utakuwa umepokea baruapepe kama hii pichani

Inamaanisha kuwa umepewa “paid subscription” ya bure kwa wiki moja. Endapo utahitaji kuwa “paid subscriber” moja kwa moja basi bonyeza hicho kitufe cha “continue subscribing” na utapelekwa kwenye ukurasa huu pichani chini

Na hapo una fursa ya kuchagua “plan” unayoona inakufaa, aidha ya malipo kwa mwezi USD 5 au kwa mwaka mzima USD 50. Lakini pia unaweza kuwa “mwanachama mwanzilishi” wa kijarida hiki kwa kuchangia USD 100.

Siku njema.

Jasusi/mtumishi wako 😎

Share this post
Mchungaji Msigwa 'Aamuriwa' na Lema Kufuta Twiti Iliyoshauri Kuwa Chenge Ndio Anafaa Kuwa Spika, Aifuta, Kisha Airejesha 'Kiaina.'
www.baruayachahali.com
TopNewCommunity

No posts

Ready for more?

© 2022 Evarist Chahali
Privacy ∙ Terms ∙ Collection notice
Publish on Substack Get the app
Substack is the home for great writing