Mashujaa wa GEN-Z TANZANIA Waliowezesha NO REFORMS NO ELECTION Waibuka na USHINDI Mnono: Wasababisha BASHITE Akose Uwaziri Mkuu
Moja ya mafanikio makubwa kabisa ya maandamano ya Gen-Z wa Tanzania yaliyofanyika kuanzia Oktoba 29, 2025 ni kuwezesha ajenda ya NO REFORMS NO ELECTION kutimia.
Japo awali ajenda hiyo ilianzishwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), baadaye vijana wa Gen-Z waliichukua na kuiingiza kuwa moja ya ajenda zao kwa ajili ya maandamano waliyopanga kuyafanya siku ya uchaguzi mkuu, yaani Oktoba 29 lengo likiwa ni kuzuwia kufanyika kwa uchaguzi huo.
Na hilo lilifanikiwa kwa asilimia 97.8! Wakati idadi ya Gen-Z ikitawala mitaani katika maeneo mbalimbali ya Tanzania, idadi kubwa ya vituo vya kupiga kura vilikuwa tupu.
Kwahiyo, kwa vile Chama cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake walikataa kufanya mabadiliko ya sheria za uchaguzi (NO REFORMS), hakukuwa na njia nyingine zaidi ya kuziwia uchaguzi huo (NO ELECTION).
USHINDI WA PILI
Lakini licha ya mafanikio hayo makubwa, mashujaa wa Gen-Z wa Tanzania wamepelekea Daudi Albert BASHITE kukosa Uwaziri Mkuu.
Iko hivi: Bashite alimhakikishia Samia kuwa Gen-Z wasingeweza kufanya maandamano yoyote baada ya yeye Bashite kuongoza operesheni ya kuteka watu mbalimbali aliodhani ndio walikuwa wakipanga maandamano.
Lakini kwa mshangao mkubwa kwake na Samia, maelfu ya Gen-Z walijitokeza mtaani na kutikisa nchi kwa siku 5 mfululizo kabla ya Samia kuanza kuwachinja kinyama.
Taarifa zinadai kuwa idadi ya waliouawa hadi sasa inazidi watu ELFU KUMI.
Hata hivyo, japo inatia uchungu sana kuona amsiaha ya vijana hao mashujaa yakikatishwa na Samia, ukweli unabaki kuwa wamepanda mbegu ya mabadiliko ambayo kwa hakika inaifanya Tanzania kuwa yenye mwelekeo mwema kuliko ilivyo sasa au huko nyuma.
Damu yao haijapotea bure. Ni suala la muda tu kabla ya walioyapigania kuanza kuonekana.


