Barua Ya Chahali

Share this post
Maridhiano Feki Kati Ya Chadema Na Jiwe
www.baruayachahali.com

Maridhiano Feki Kati Ya Chadema Na Jiwe

Evarist Chahali
Dec 12, 2019
2
Share this post
Maridhiano Feki Kati Ya Chadema Na Jiwe
www.baruayachahali.com

Kabla sijaingia kwa undani kwenye mada hii naomba kutumia fursa hii kukukaribisha ujipatie moja ya kazi zangu bora kabisa, kitabu cha kilektronikia kinachozungumzia kwa kina mazingira yaliyopelekea kufukuzwa kazi kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Dkt Modestus Kipilimba.

Umuhimu wa kitabu hiki upo sio tu katika kuweka rekodi sawa na kumbukumbu kuhusu tukio hilo la kihistoria - kamwe haijatokea nchini Tanzania kwa Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa kufukuzwa kazi - bali pia ni ukweli kwamba kwa mazingira yaliyopo, sio rahisikwa wewe mdau kupata fursa ya kukutana namaelezo ya kina kuhusu tukio hilo hasa kwa vile vyombo vya habari vimezibwa mdomo kwa nguvu kubwa na serikali ya Jiwe.

Na kama ushajipatia nakala yako, basi si vibaya ukimhamasisha mwezio nae asikose uhondo huo. Pia kuna ofa hii hapa chini ya kufungia mwaka endapo utahitaji

Baada ya matangazo haya mawili, twende kwenye mada. Uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ulitangaza majuzi kuwa ungeshirikia sherehe za maadhimisho ya miaka 58 ya “uhuru wa Tanganyika.”

Binafsi, hofu yangu kubwa ilikuwa kwamba Jiwe angeweza kutumia fursa hiyo kuwadhalilisha viongozi hao wa Chadema kama ambavyo amekuwa akifanya mara nyingi kila inapotokea viongozi wa upinzani kushiriki katika hafla ambazo Jiwe ni mgeni rasmi.

Twitter avatar for @ChahaliEvarist Chahali @Chahali
I just hope baadaye hatutosikia malalamiko ya "tumedhalilishwa."
Image

December 8th 2019

3 Retweets13 Likes

Kwamba Jiwe ana chuki kali dhidi ya wapinzani hususan wa Chadema, hilo halihitaji uelewa japo kidogo wa siasa za Tanzania kwani ni jambo la wazi.

Sijui kwanini sikujihangaisha kujiuliza, “hivi jeuri hii ya akina Mbowe kwenda kuungana na Jiwe Mwanza wameitoa wapi?” Maana laiti ningejiuliza hivyo basi nisingeshangazwa na kauli ya Mbowe kuhusu anachokiita MARIDHIANO.

Twitter avatar for @millardayomillardayo @millardayo
“Nimekuja kushiriki Sherehe hizi za Miaka 58 ya Uhuru kama uthibitisho wa ulazima wa kuwepo maridhiano, upendo na mshikamano katika Taifa letu, namuomba Mungu siku ya leo ikafungue milango tuweze kuishi kama Taifa linalopendana, tuvumiliane, tukosoane, turuhusu Demokrasia”-MBOWE
Image
Image

December 9th 2019

78 Retweets913 Likes

Tatizo kubwa kuhusu tamko hilo la Mbowe ambalo ninaamini ndio msimamo wa Chadema kwa ujumla lipo kwenye ukweli kwamba ili pawepo MARIDHIANO basi ni lazima pande husika ZIRIDHIE. Sasa tunaweza kurahisisha mahesabu kusema pande husika hapo ni Chadema na CCM. Je CCM wana dalili zozote za kuridhia “kupatana” na Chadema? Hili nalo halihitaji uelewa mkubwa wa siasa za Tanzania.

Twitter avatar for @zittokabweZitto Kabwe Ruyagwa @zittokabwe
@IAMartin_ Shida kubwa hatusomi na kujifunza. Zanzibar walipata maridhiano kwa sababu kuna mizania sawa. Maridhiano huombwa na mkandamizaji baada ya kufikishwa mahala hana njia. Mkandamizwaji akiomba Maridhiano anaomba poo. Kama Mimi niliomba ni lazima mfuate kama nyumbu? La hasha.

December 9th 2019

3 Retweets28 Likes

Lakini kiukweli pande husika sio Chadema na CCM tu bali ni complicated zaidi. Kwa upande mmoja ni mfumo kandamizi dhidi ya haki za kidemokrasia, hili ni zaidiy a Chadema na CCM.

Kwa upande mwingine ni CCM dhidi ya mfumo wa siasa za upinzani, ambapo kwa tunaofuatilia siasa hizo tangu ziasisiwe mwaka 1992, hakuna wakati wowote ambapo chama hicho tawala kimeonyesha kwa dhati kuukubali mfumo huo.

Tofauti pekee kati ya zama za Mwinyi, Mkapa na Kikwete vs hii zama ya Jiwe ni kwamba angalau hao watangulizi walijitahidi kuficha chuki zao dhidi ya upinzani, ilhali Jiwe hanamuda wa kuficha chuki zake.

Japo wazo la Chadema kutana maridhiano ni zuri lakini haliwezekani katika mazingira yaliyopo. Ni hivi, CCM has everything to lose endapo haki itatendeka kwa vyama vya upinzani. CCM sio wajinga, wanafahamu fika uhusika wao katika kuikongoroa Tanzania yetu. Wanatambua fika kuwa hawawezi kukwepa lawama kuhusu “vyuma kukaza.” Lakini CCM pia sio wajinga wa kupita huku na kule kuwaambia Watanzania kuwa “jamani eee, sie ndio tumewekeza nguvu kwenye ununuzi wa bombadia na ujenzi wa Stigla na SGR huku madawa yakianza kuuzwa kwa bima za vifurushi, huku watoto lukuki wakifaulu lakini wakiishia kukosa nafasi za kuendelea na masomo, huku umasikini ukizidi kuongezeka, na ukweli mwingine mchungu kama huo.

Watu pekee wanaoweza kuongea hayo ni akina Mbowe na wapinzani wenzake. Sasa kwa CCM kutoa uhuru huo maana yake itakuwa imeruhusu “kampeni chafu” dhidi yake. Na katika mazingira ya kawaida tu, si rahisi kumruhusu adui yako akuchafue kwa hiari yako.

Lakini tatizo lililopo zama hizi ni kubwa zaidi. Tuna mtawala anayedhamiria kwa dhati kutawala milele kwa mkono wa chuma. Mtawala huyo amefanikiwa kuua uhuruwa vyombo vya habari, kuua haki ya wanachi kusikia matangazo ya Bunge, kuua haki za vyama vya upinzani kufanya shughuli zao halali za kisiasa -mikutano na maandamano- na mengineyo mengi.

Kiongozi wa aina hii haoni incentive yoyote katika kinachoitwa MARIDHIANO.

Twitter avatar for @ChahaliEvarist Chahali @Chahali
Unajua nini cha kusikitisha zaidi kuliko imani hii fyongo ya Jiwe? (1) Hakuna incentive yoyote ya kumfanya abadili imani hiyo (can't blame him really because if it's working for him, why fix it?) (2) Ndugu zetu wa upinzani wamekubali kuwa hii ndio stahili yao.
Image

November 28th 2019

3 Retweets13 Likes

Ukiangalia juujuu unaweza kudhani kinachoombwa na Mbowe ni ruhusa ya Jiwe kwamba vyama vya upinzani viruhusiwe kufanya shughuli zake halali za kisiasa. Kwanza hapo tu Mbowe yupo wrong kwa sababu HAKI HAIOMBWI

Twitter avatar for @ChahaliEvarist Chahali @Chahali
"Haki haiombwi na wala haki haitolewi kama fadhila au zawadi. Haki hudaiwa...hata kwa nguvu ikibidi" ~ Marehemu Prof Kighoma Ali Malima

July 28th 2013

1 Retweet

Na kuomba haki ni sawa na kuomba/kukubali pungufu ya stahili, na ni muhimu kuelewa athari za kuomba/kukubali pungufu ya unachostahili

Twitter avatar for @ChahaliEvarist Chahali @Chahali
Yea, never settle for less than you deserve. That's the rule to obey. #LifehacksInSwahili
Instagram.com/evarist_chahali
Image

April 20th 2018

2 Retweets3 Likes

Naam, Mbowe na wenzie wanaweza kukubaliwa ombi lao la MARIDHIANO. Lakini kwenye sosholojia tunafundishwa kuwa msingi wa mahusiano ya binadamu huelemea kwenye “nipe nikupe.” Kwa mantiki hiyo, yayumkinika kuamini kuwa hata kama Jiwe akikubali ombi hilo la Chadema, kuna kitu atakachohitaji kutoka kwao.

Hint kuhusu kitu hicho ipo kwenye tweet hii ya Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT- Wazalendo

Twitter avatar for @zittokabweZitto Kabwe Ruyagwa @zittokabwe
Wana historia mnakumbuka, Samora Machel alifanya kosa kubwa kusaini Nkomati Accord na Serikali ya Makaburu wa Afrika Kusini licha ya kushauriwa na Marais wenzake asifanye hivyo. Akawa mbishi. Miaka 2 baadaye Makaburu walimwua. ANC walipata tabu sana 1984-1987. TUJIFUNZE

December 9th 2019

42 Retweets574 Likes

Lengo la Jiwe kuuangamiza upinzani sio tu lipo palepale bali sasa limerahisishwa na akina Mbowe. Kwanini? Kwa sababu katika hiyo “nipe nikupe” Mbowe na wenzake watapewa conditions ambazo essentially ni sawa na kujifunga kitanzi wenyewe.

Kwa sababu Jiwe sio mtu katili tu balipia si mjinga wa kuwaruhusu Chadema au wapinzani kwa ujumla wapate mazingira mazuri ya “kumkalia kooni” kuhusu yu wapi Ben Saanane, yu wapi Azory Gwanda, watu wangapi waliuawa huko MKIRU, ni nani alipanga njama za kumuua Tundu Lissu… orodha ni ndefu.

Lakini baya zaidi katika kinachoitwa MARIDHIANO ni siri iliyofichika katika “sarakasi” hiyo. Kwa mujibu wa taarifa, kinachotafutwa na viongozi hao wa Chadema ni “genge hilo kuachiwa na Jiwe nafasi kadhaa za ubunge hapo mwakani” na si kuruhusiwa kwa siasa za upinzani bila masharti.

Naomba niishie hapa kwa sasa, nikiahidi kuendelea na mada hii siku nyingine. Moja ninaloweza kubashiri bila shaka ni kwamba matokeo ya MARIDHIANO yataigharimu Chadema big time.

Lakini licha ya kukigharimu chama hicho, kitendo cha Mbowe na wenzake “kakaa jukwaa moja na Jiwe wiki chache tu baada ya uhuni mkubwa wa kihistoria uliopelekea CCM kujipa ushindi wa asilimia 99.9 kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa” ni usaliti wa hali ya juu.

Lakini angalau sasa tunaweza kuelewa kuhusu HAMA HAMA inayoendelea huko Chadema, bila kusahau kwanini chama hicho kimetulia kana kwamba hakikuhujumiwa kwenye uchaguzi wa juzi wa serikali za mitaa.

Mwisho I wish tungeweza pia kusikia mitazamo ya akina Ben Saanane au marehemu Mawazo, Luena na (Katibu Kata Hananasifu) Daniel - baadhi ya wahanga wa siasa za chuki zinazoendelezwa na Jiwe ambazo sasa Chadema wanataka KURIDHIANA nazo.

Comment
Share
Share this post
Maridhiano Feki Kati Ya Chadema Na Jiwe
www.baruayachahali.com

Create your profile

0 subscriptions will be displayed on your profile (edit)

Skip for now

Only paid subscribers can comment on this post

Already a paid subscriber? Sign in

Check your email

For your security, we need to re-authenticate you.

Click the link we sent to , or click here to sign in.

TopNewCommunity

No posts

Ready for more?

© 2022 Evarist Chahali
Privacy ∙ Terms ∙ Collection notice
Publish on Substack Get the app
Substack is the home for great writing