Barua Ya Chahali

Share this post
Maridhiano Aliyoomba Mbowe "Yaanza Kuzaa Matunda"
www.baruayachahali.com

Maridhiano Aliyoomba Mbowe "Yaanza Kuzaa Matunda"

Evarist Chahali
Dec 18, 2019
2
Share this post
Maridhiano Aliyoomba Mbowe "Yaanza Kuzaa Matunda"
www.baruayachahali.com

Not so fast. Baadhi yetu tuliposikia ile kauli ya Mbowe kuhusu MARADHIANO tulijua anapoteza muda wake tu. Nilieleza kwa kirefu kuhusu MARADHIANO kwenye makala hii

Na kabla wiki haijapita tangu Mbowe atoe rai hiyo kwa Jiwe, Jeshi la Polisi kwa maelekezo ya serikali ya CCM yamefikisha ujumbe kwa Mbowe na Chadema kwa ujumla kuwa hawana muda wa MARADHIANO na chama hicho, kama inavyojitanabaisha kwenye habari hii

Polisi Tanzania wataka bendera za Chadema zishushwe

TUESDAY DECEMBER 17 2019

Kwa ufupi

Polisi wafika eneo la ukumbi wa Mlimani City ambao Chadema wanakofanya mikutano yao na kuamuru viongozi wa chama hicho kushusha bendera walizoziweka kando kando barabara ya Sam Nujoma.

By Mwandishi Wetu, Mwananchi []

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi limefika katika ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam likiwataka viongozi wa chama kikuu cha upinzani cha Tanzania (Chadema) kushusha bendera za chama hicho zilizowekwa barabara ya Sam Nujoma.

Bendera hizo zimewekwa kuanzia Superstar hadi mzunguko karibia na Kanisa na Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) ambapo chama hicho kinafanya mikutano ya uchaguzi katika ukumbi wa Mlimani City iliyoanza Desemba 9, 2019 na itahitimishwa keshokutwa Alhamisi ya Desemba 19, 2019

Askari polisi sita waliokuwa kwenye magari mawili aina ya Noah na Land Cruiser  waliutaka uongozi Chadema kushusha bendera hizo kwa maelezo kuwa ni amri kutoka kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, Beatrice Dominic.

Mapema leo Jumanne Desemba 17, 2019 Dominic alikiandikia barua chama akikitaka kuzishusha bendera hizo zilizowekwa eneo la bustani pembezoni mwa barabara hiyo akieleza zimewekwa kama matangazo au mabango kinyume cha utaratibu.

Polisi hao walikutana na viongozi mbalimbali wa Chadema akiwemo, Mkurugenzi wa Itifaki, Uenezi, Mawasiliano  na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema, Meya wa Ubungo, Boniface Jacob,  Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema katika mazungumzo yao viongozi hao waligoma kuzishusha bendera hizo.

"Wametuambia tuzishushe halafu kesho tuzipandishe, tumewaambia hilo haliwezekani, labda washushe wao," amesema Jacob.

Habari zinazohusiana na hii

  • Chadema wapewa saa mbili kuondoa bendera za chama hicho barabarani

Naye Mrema amesema "Msimamo wa chama hatushushi bendera kwa sababu hatuvunji sheria kama chama cha siasa. Wakitaka wazishushe wao," amasema Mrema akiwaambia baadhi ya wanachama wa chama hicho waliokuwa wakisubiri mrejesho wa suala hilo.

Baada ya Mrema kutoa kauli hiyo baadhi ya wanachama walisikika wakiwahamasisha wenzao kutoka nje ya ukumbi kwenda barabarani kulinda bendera hizo.

Mpaka saa 2:30 asubuhi polisi walikuwapo eneo hilo huku baadhi ya wanachama wakienda barabara kulinda bendera hizo.

Nadhani kila mwenye akili timamu ataelewa nilichotanabaisha kwenye makala kuhusu MARADHIANO na kuelewa kwanini it was a bad idea.

Nimalizie kwa tangazo kuhusu moja ya kazi zangu bora kabisa, kitabu cha kilektronikia kinachozungumzia kwa kina mazingira yaliyopelekea kufukuzwa kazi kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Dkt Modestus Kipilimba.

Ndimi mtumishi wako,

Evarist Chahali

Comment
Share
Share this post
Maridhiano Aliyoomba Mbowe "Yaanza Kuzaa Matunda"
www.baruayachahali.com

Create your profile

0 subscriptions will be displayed on your profile (edit)

Skip for now

Only paid subscribers can comment on this post

Already a paid subscriber? Sign in

Check your email

For your security, we need to re-authenticate you.

Click the link we sent to , or click here to sign in.

TopNewCommunity

No posts

Ready for more?

© 2022 Evarist Chahali
Privacy ∙ Terms ∙ Collection notice
Publish on Substack Get the app
Substack is the home for great writing