Makonda "Kikaangoni" Baada ya Nape Kurudishiwa Uwaziri wa Habari na Ridhiwani Kuteuliwa Naibu Waziri
Mustakabali wa Paul Makonda, mkuu wa zamani wa Mkoa wa Dar es Salaam, ni tete kufuatia wanasiasa wawili aliowanyanyasa wakati akiwa madarakani, Nape Nnauye na Ridhiwani Kikwete kuingizwa kwenye kabineti ya Mama Samia katika mabadiliko yaliyotangazwa Jumamosi.
Nape ameteuliwa kuwa Waziri mpya wa Habari, Mawasiliano na TEHAMA, ilhali Ridhiwani amepewa Unaibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Lakini hata kabla ya teuzi hizo, kulikuwa na jaribio la kumfungulia kesi Makonda kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka yake, kufuatia uvamizi aliofanya kwenye kituo cha habari cha Clouds jijini Dar es Salaam, saa 4 unusu usiku, Machi 17, 2017