Makala Ya Wazi Ya #BaruaYaShushushu

Dondoo Mbili za Kijasusi

Karibu katika toleo hili la wazi (kwa maana ya kutumwa kwa wanachama na wasio wanachama wa #BaruaYaChahali yenye jumla ya vijarida vinne kwa wiki), toleo ambalo pia ni la mwisho kwa mwaka huu 2019.

Katika toleo hili ninagusia vitu viwili vya kijasusi. Kimoja nilikigusia Desemba mwaka jana kupitia mtadao wa kijamii wa Twitter

Ni rahisi sana kuwahujumu Watanzania kwa kutumia mbinu rahisi tu za kishushushu. Sijui ni kwa sababu nchi imekuwa kwenye amani muda mrefu au kwa vile vipaumbele vya Watanzania wengi ni kwenye ubuyu, lakini kwa hakika watu wengi sio tu hawapo makini kiusalama bali hawana muda kutafakari mara mbili kuhusu usalama wao.

Binafsi nilijaribuhuko nyuma kutoa elimu ya bure kuhusu usalama “wa mtaani” na “wa mtandaoni,” lakini kuwatumikia Watanzania ni kama kubeba gunia la misumari. Unajituma kudhani unachofanya kina umuhimu kwa watu lakini kinaishia kupuuzwa tu. Eventually unaamua kuachana na huo “utumishi wa bure kwa umma.”

Katika twiti hiyo nilitanabaisha kwamba huo mkusanyiko wa “watu waliofahamiana kupitia Twitter,” - hilo bonanza - japo ni mzuri kwa minajili ya kutengeneza marafiki na ku-network, lakini si mwafaka sana kwa mtu mwenye kuchukua tahadhari kuhusu usalama wake.

Ni hivi, Tanzania ni “dola ya kiintelijensia,” kwa kimombo wanaita “intelligence state.” Ni kama Russia. Ni kama Rwanda. Ni nchi ambayo Idara ya Usalama wa Taifa imepenyeza watu takriban kwenye kila eneo.

Ninaposema “watu” simaanishia maafisa wa taasisi hiyo bali watu ambao mtaani mnawaita “infoma” (informers) ilhali nenola kishushushu ni “watoa habari” kwa kimombo “intelligence sources” au kwa kifupi “sources.”

Kwa kawaida Idara za Usalama wa Taifa popote pale dunianihuwa na maafisa wachache lakini kila afisa huwa na mtandao mkubwa wa watu wanaompatia taarifa.

Kwa mfano, “shirika la ushushushu wa ndani” kwa hapa Uingereza - MI5 - lina takriban maafisa 4,000 tu katika taifa hili lenye zaidi ya watu milioni 66.

Kwa huko Marekani, taifa lenye watu zaidi ya milioni 327, shirika la ujasusi la nchi hiyo (CIA) ina takriban maafisa 20,000 tu.

Siwezi kutaja idadi ya maafisa wa “kitengo” kwa sababu zilizo wazi, lakini “mtaji” mkubwa kwenye raslimaliwatu ya “kitengo” ni kwenye hao “watoa habari.” Na hawa wamezagaa kila kona.

Na kana kwamba hiyo haitoshi, Jiwe alipoingia madarakani akawaleta “watu wake” wa MATAGA ambao licha ya mapungufu yao lukuki kiutendaji, wamejazana vya kutosha kwenye mitandao ya kijamii.

Kwahiyo kunapotokea hafla ya watu wanaotoka kwenye mitandao ya kijamii - kama hilo bonanza la TOT - sio tu kwamba “kitengo” kitamwaga watu wake - both maafisa na hao watoa habari - bali pia kinakuwa kinawinda fursa za kunasa watu wanaoweza kusaidia “kumjua nani ni nani” au kupata taarifa za “kuwanasa watu wanaowindwa.”

Dondoo ya pili inajieleza kwenye twiti zangu hizi mbili

Na kabla ya twiti hizo nilitoa ushauri wa bure kuhusu “watu tunaofahamiana nao mitandaoni”

Naam, haya mahusiano ya mtandaoni yanahitaji umakini. Licha ya fursa luluki zinazopatikana mtandaoni, kuna “mabaya” mengi tu yanayokusubiri “ukosee njia tu uumizwe.”

Ukisikiliza maelezo ya Prof Assad na kurejea “uzushi” kuwa alikuwa ametekwa, hutoshindwa kuelewa logic yangu kuhusu “mchezo” unaoendelea kuhusiana na sakata la #WatuWasiojulikana.

Nimalizie kwa tangazo hili la vitabu vyangu

Ndimi jasusi wako,

Evarist Chahali