Makala Ya Wazi: Uamuzi wa Chadema Kujitoa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Kwamba uchaguzi huu wa serikali za mitaa ni uhuni wa kidemokrasia, hilo wala si jambo linalohitaji mjadala. Labda tunachoweza ku-note ni kwamba uchaguzi huu utaingia kwenye historia ya taifa letu, pengine kama ishara rasmi ya kupulizwa kipyenga cha utawala wa kidikteta.

Kwamba wapinzani wana kila sababu na haki kulalamikia na Hata kususia uchaguzi huo nalo si jambo linalohitaji mjadala.

Hata hivyo, uamuzi wa Chadema kujitoa kwenye uchaguzi huo HIVI SASA una walakini mkubwa.

Najua makada wa Chadema hawana tofauti na wa CCM when it comes to kukosolewa. Sintoshangaa kupokea “pongezi za matusi” kutokana na makala hii.

Chadema walipaswa kuchukua hatua kabla ya kufanya hiyo “nataka sitaki.”

Hivi kweli Chadema na wapinzani kwa ujumla walitegemea mabadiliko yoyote kinyume na ilivyojiri katika chaguzi zote tangu Jiwe aingie madarakani?

Je chama hicho kikuu cha upinzani kiliingia kwenye uchaguzi huo bila kufanya tathmini yoyote ile?

Niliwahi kuandika makala moja huko nyuma kuhusu “catch 22” inayowakabili wapinzani kwenye hizi chaguzi.

Ni kwamba wapinzani wakisusa, “CCM watakula.” Na wapinzani wakishiriki, wanahalalisha haramu.

Kwahiyo japo Chadema inaweza kukosolewa kwa kujitoa kwenye uchaguzi huo muda huu na sio tangu mwanzoni, bado uamuzi wa kususia uchaguzi ungeweza kutozaa matunda kusudiwa.

Which brings us to a critical question: NINI KIFANYIKE? Mwarobaini wa haya yote ni kile kilichozaa UKAWA, dhamira ya dhati kabisa kudai katiba mpya.

Unfortunately, madai ya katiba mpya yamekufa kifo cha asili. There is no way Jiwe ataruhusu wapinzani kufanya shughuli zap halali za kisiasa BILA KULAZIMISHWA afanye hivyo.

Nadhani tatizo linalowakabili wapinzani wetu bi ku-underestimate dhamira ya Jiwe kuangamiza upinzani nje na ndani ya chama chake, hatua muhimu kuelekea udikteta kamili.

Kwa kuhitimisha, badala ya kutumia nguvu nyingi kulalamika kuhusu uhuni huu unaoendelea ni muhimu kwa wapinzani na Watanzania kwa ujumla kudai katiba mpya itakayotoa haki na fursa sawa za kidemokrasia kwa vyama na wananchi.

Ningependa kusikia maoni yako. Niandikie HAPA.

Mwisho, tangazo kidogo.

Unaweza kujiunga kuwa “mwanachama” wa #BaruaYaChahali yenye mkusanyiko wa vijarida vinne kwa wiki, kwa KUBONYEZA HAPA.

Na endapo hutaki kuendelea kutumiwa baruapepe kutoka kwangu, JIONDOE HAPA.

Na vitabu hivi 👇 bado vinapatikana

Ndimi mtumishi wako,

Evarist Chahali