Makala Ya Wazi: Tunakoelekea Sio Kuzuri

Sijui Tanzania yetu inaelekea wapi lakini uhuni unaoendelea kufanywa na Jiwe kupitia mbwa wake Musiba ni hatari kwa mustakabali wa Taifa letu.

Musiba anatuweka njia panda ambapo tukimwongelea sana tunakuwa tunampa umuhimu asiostahili, lakini tukimkalia kimya anaweza kudhani aidha tunamuogopa au tunaafikiana nae.

Lakini pia katika hali isiyitarajiwa, Musiba ameweza kutuweka pamoja hata watu tuliowahi kufarakana huko nyuma. Kwa mfano, katika toleo la leo la moja ya magazeti yake lukuki, ameweka habari kuhusu huyu kijana ambaye mie mtumishi wako nililazimika kumbloku baada ya usumbufu mwingi aliokuwa ananifanyia huko Twitter.

Lakini hata kama kijana huyo angekuwa amenifanyia baya gani basi nisingefurahia unyama huu unaofanywa na Musiba.

Lakini pia kuna fundisho hapa. Watu wengi walifurahi sana kila walipoona jina la mie mtumishi wako kwenye hizo takataka za Musiba. Badala ya kumkemea, wao waliona ananikomoa. Walichosahau ni msemo “mwenzio akinyolewa wewe tia maji. “

Na hili linapaswa kuleta mwamko kwa kila mmoja wenu kwa sababu ipo siku nanyi mwaweza kuwa wahanga wa uhuni huu.

Kwa upande mwingine, kuna mambo makuu mawili yanayomwongezea ari Musiba

Lakini tukiweka hilo kando, kuna taarifa ambayo kwa hakika imenipa hofu kubwa.

Kwa vile Jiwe hajawahi kumkemea Musiba, na kwa vile kuna kila ushahidi wa wazi kuwa Musiba ni mbwa tu ila mwenye mbwa ni Jiwe, kwanini tishio hilo la Musiba kwa majaji lisiwatishe majaji?

Na pengine ndio maana licha ya kufunguliwa kesi ya madai na Membe, mbwa huyo ameendelea kumshushia Membe tuhuma nzito mfululizo.

Naomba makala hii ikusaidie kuamsha tafakuri kuhusu mustakabali wa Taifa letu.

Nimalizie kwa tangazo hili kuwakaribisha nyote ambao hamjajiunga na #BaruaYaChahali

Jinsi ya kujiunga: Uanachama kwa mwaka mzima ni sh100,00 au sh 10,000 kwa mwezi. Tuma mchango wako kwa m-pesa namba 0767632516 (jina Khadija Katule). Kwa walio nje ya Tanzania, unaweza kuchangia kwa KUBONYEZA HAPA.

Endapo unataka kuondolewa kwenye orodha ya wanaotumiwa #BaruaYaChahali JIONDOE HAPA.

Ndimi mtumishi wako

Evarist Chahali