Makala Ya Wazi: Tafsiri Ya Barua Ya Makamba, Kinana Kuhusu Musiba

Kwenye Ushushushu, La Muhimu Zaidi Huwa Linalosikika/Linalosomeka Bila Kutamkwa/Kuandikwa

Kwanza naomba kutanabaisha kuwa mtumishi wenu anawajali nyote - mnaoiunga mkono #BaruaYaChahali kwa michango ya uanachama na “mliosusa.” Na ndio maana yanapojiri matukio mazito kama hili la “Barua ya Makamba na Kinana kuhusu Musiba” mtumishi wako nalazimika kuweka majukum8uu yangu kando ili kukupatia uchambuzi kama huu ambao si rahisi kuupata kwingineko.

Kama hujaona vichwa vya habari vya magazeti ya leo, basi ngoja nikusaidia kabla hatujaenda kwenye uchambuzi wa kina.

Naam, hatimaye chatu aliyefugwa akidhaniwa angewang’ata “Watu Hatari” (akina Chahali) tu, sasa anataka kuwameza wanaommiliki. Wanasema chatu ana tabia moja mbaya. Ukimnyima chakula atapatwa na njaa na ataishia kukumeza. Ukimlisha mlo mzuri atanawiri, na kuwa mkubwa kiasi ataweza kukumeza kirahisi. Ndio ilivyo kwa Musiba.

Na kama hujafanikiwa kuiona barua ya Makamba na Kinana basi nakuwekea hapa chini katika tweet ifuatayo

Kama nilivyotanabaisha hapo mwanzo, sie majasusi tunaposoma/tunaposikia kitu huwa tunajibidiisha zaidi kubaini “yanayosomeka bila kuandikwa na yanayosikika bila kusemwa.” Na katika barua ya Makamaba na Kinana, kinachosomeka bila kuandikwa/ kinachosikika bila kusemwa ni kwamba ANAYEMPA JEURI MUSIBA, na ambaye pia ANAMTUMA ni Jiwe.

Na kama unafuatilia kwa karibu matamko ya Musiba (yanaumiza sana kusikia kama una uchungu wa dhati kwa nchi yetu) si vigumu kubaini kuwa “yanayosikika bila kusemwa” ni pamoja na tuhuma dhidi ya Jk, Mkapa na Mwinyi - japo mlengwa mkubwa ni JK.

Tatizo la Jiwe ni imani yake kuwa Jk anapanga kumpindua. Hili limekuwa likimsumbua kwa muda mrefu sana. Na ndilo linachangia hofu yake kuhusu Membe. Na hata hawa akina Makamba na Kinana, wanaandamwa kwa ajili ya Jk.

Kingine kinachompa mchecheto Jiwe hadi kumtumia Musiba ni hofu ya kile alichotendewa Lowassa. Maana bila nguvu ya Jk, Mkapa na Mwinyi - pamoja na wakongwe kama Kinana, Jiwe angeusikia urais kwenye bomba tu.

Lakini haya yote ni matokeo ya siasa za rafu ndani ya CCM. Na haya hayakuanza leo. Mwaka 1995, Nyerere aliwawekea zengwe Jk na Lowassa (angalau ilikuwa kwa nia nzuri). Mwaka 2005, Jk, Lowassa na Rostam walimwekea zengwe Dkt Salim Ahmed Salim (katika moja ya kampeni chafu kabisa katika historia ya Tanzania). Na mwaka 2015 Jk, akishirikiana na Mkapa na Mwinyi walimwekea zengwe Lowassa (partly kwa sababu nzuri, partly kwa uhuni tu).

Kwahiyo, kwa kifupi, barua hiyo ya Makamba na Kinana ni malalamiko ya moja kwa moja kwa Jiwe. Ni jinsi ujumbe huo ullivyovujishwa makusudi kwenye vyombo vya habari ina maana moja tu, kwamba hii sasa ni “political street fight” na kwa wanaofahamu kuhusu “ngumi za kitaa,” huwa hakuna sheria wala kanuni. Zinaweza kudumu mwaka mzima, au dakika chache tu.

Tatizo kubwa kwa Jiwe ni kupenda kutenegeneza maadui bila sababu za msingi. Sasa aezungukwa na maadui wenye nguvu, wenye uzoefu mkubwa wa mbinu safi na chafu za siasa, ilhali yeye si mwanasiasa mzoefu, na laiti angekuwa na washauri wema, angeachana na mkakati huu wa kumtumia Musiba kama “attack dog” wake.

Uchambuzi huu ni endelevu. Bado nakusanya data kutoka kwa vyanzo vyangu.

Nimalizie kwa tangazo lifuatalo

Uanachama kwa mwaka mzima ni sh100,00 au sh 10,000 kwa mwezi. Tuma mchango wako kwa m-pesa namba 0767632516 (jina Khadija Katule). Kwa walio nje ya Tanzania, unaweza kuchangia kwa KUBONYEZA HAPA.

Endapo unataka kuondolewa kwenye orodha ya wanaotumiwa #BaruaYaChahali JIONDOE HAPA.

Ndimi mtumishi wako

Evarist Chahali