Makala Ya Wazi: Rais Magufuli Amesema UONGO Kuhusu Dkt Mwele

Madai Yake Kuwa Dkt Mwele Aliteuliwa Shirika la Afya Duniani Baada Ya Wiki Moja Ni Urongo, He Should Be Ashamed of Himself

Kwamba Rais Magufuli ni mtu mwenye roho mbaya wala sio jambo la kushangaza. Na wa kubebeshwa lawama kuhusu mtu huyu mwenye roho mbaya kuja kuwa katika nafasi isiyostahili kabisa kushikwa na mtumwenye roho mbaya - nafasi ya urais - ni Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, na wastaafu wenzie Ben Mkapa na Ali Hassan Mwinyi.

Kwanini wanapaswa kubebeshwa lawama? Kwa sababu licha ya kufahamu fika kuwa Magufuli ni mtu asiyetabirika, mwenye hasira za ajabu ajabu, muumini wa ubabe badala ya busara, na mpenda chuki, visasi na vinyongo, wao “walisimama nae” ili kumzuwia Lowassa asiwe Rais.

Sawa, Lowassa nae hakuwa mtu stahili kushika nafasi ya urais lakini bado kulikuwa na wagombea wengine ambao kwa hakika wangeweza kuwa marais wazuri kuliko hili balaa tulilonalo sasa.

Mtu mmoja aliyekuwemo kwenye msafara wa kampeni za Magufuli mwaka 2015 alimsikia akitamka mara kwa mara “kwanini msimuue/msiwaue tu?” kila wanasiasa “wakorofi” wa upinzani walipokuwa wanaongelewa. Na hakuwa anaongea kama mzaha bali alionyesha kwa dhati kuamini kuwa njia mwafaka ya kudili na wapinzani ni KUWAUA.

Na Magufuli ana bahati sana kwani mpaka muda huu amefanikiwa kabisa kuzima taarifa za unyama alioufanya huko MKIRU (Mkuranga, Kibiti na Rufiji). Lakini pengine sio bahati mbali uzembe tu wa Watanzania kufuatilia mambo. Na pengine wa kulaumiwa ni ndugu zangu Waislam kwa sababu takriban asilimia 99 ya wahanga wa unyama wa MKIRU walikuwa Waislamu. Hata hivyo katika dunia hii ya kidigitali, naamini ipo siku ukweli utafahamika na hapo ndipo Watanzania watamwelewa vizuri huyu mtu katili.

Juzi, siku moja baada ya kuunga mkono uvunjifu wa sheria uliofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Chalamila aliyejipa jukumuu la ualimu na kuwacharaza viboko wanafunzi wa serkondari moja huko Mbeya, Magufuli alikurupuka na kuongea vitu vya ajabu kabisa.

Katika kukurupuka huko kwa mara nyingine, alishindwa kuzuwia chuki zake dhidi ya mmoja wa Watanzania wachache wanaotuwakilisha vema kimataifa, Dokta Mwele Malecela.

Kibaya zaidi, chuki ya Magufuli dhidi ya Dokta Mwele iliambatana na uongo wa mchana kweupe. Wakati Magufuli akidai kuwa “Ndiyo maana baada ya kumfuta kazi WIKI MOJA BAADAYE waliomtumia walimpa kibarua kingine.” Huu ni UONGO WA MCHANA KWEUPE, na haipendezi kuwa na Rais muongo.

Mlolongo wa matukio upo hivi

Magufuli alimtoa Dokta Mwele madarakani tarehe Desemba 16, 2016

Image

Na kwa vile Mungu sio Magufuli, Dokta Mwele alifanikiwa kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa vituo vya Kudhibiti na Kuzuwia Magonjwa vya Afrika vya Shirika la Afya Duniani.

Hii haikuwa WIKI MOJA BAADA YA CHUKI ZA MAGUFULI kumtoa madarakani Dokta Mwele, BALI ILIKUWA ZAIDI YA MIEZI MINNE. Which means Magufuli amesema uongo, na haipendezi hata chembe kwa mkuu wa nchi kusema uongo, especially pale uongo huo unapotumika kwa ajili ya chuki na roho mbaya.

Lakini licha ya chuki na roho mbaya ya Magufuli, baadaye Dokta Mwele alipata ulaji mwingine wa hali ya juu kimataifa

Na hili ndio linamtesa Magufuli. Alidhani kutengua uteuzi wa Dokta Mwele kutapelekea mwanasayansi mtafiti huyo wa kimataifa atasugua benchi bila ajira.

Chuki ya Magufuli kwa Dokta Mwele inachangiwa na ukweli kuwa Dokta Mwele alikuwa miongoni mwa wana-CCM waliojitokeza kuchukua fomu za kuwania kuteuliwa na chama hicho kuwania nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Kwahiyo Magufuli anamuona dada huyo msomi na mwenye utu kupindukia kuwa ni tishio kwake.

Lakini bahati nzuri ni kwamba tamko lake la juzi dhidi ya Dokta Mwele limekuwa kama “kumpiga teke chura” kwani Watanzania wengi walijitokeza kwa wingi sio tu kumpa pole dada huyo bali pia kumpongeza kwa kuiwakilisha vema Tanzania kimataifa, ilhali wakimrushia lawama nyingi Magufuli kwa roho yake mbaya na kuendekeza chuki.

Lakini siku ya jana haikupita bila kituko kingine. Kwa mara ya kwanza jana alitanabaisha kuwa yeye si mtu wa kuondoka madarakani kirahisi kwa sababu anajiona ndiye pekee anayeweza kuifikisha Tanzania kunakostahili.

Huyu mtu mnaye kwa muda mrefu sana. Ila ni jukumu lenu kuchukua hatua endapo mnajali kweli mustakabali wa Tanzania yetu.

Nimalizie makala hii kwa kuwakaribisha wanaotaka kujiunga na uanachama wa #BaruaYaChahali yenye vijarida vitano kwa wiki, wanaweza kujiunga KWA KUBONYEZA HAPA (na kama unakerwa kutumiwa baruapepe kutoka kwangu, BONYEZA HAPA KUJIONDOA)

Pia kuna tangazo la vitabu

Ndimi mtumishi wako,

Evarist Chahali