Makala Ya Wazi: Ni Vigumu Kuwa Mzalendo Katika Tanzania Yetu

Vipaumbele Vya Watanzania Wengi Vipo Kwingineko

Hii ni makala ya wazi ambayo inatumwa kwa wanachama wa #BaruaYaChahali na wasio wanachama. Ndo maana inaitwa “ya wazi.” Lengo si kuwapunja waliolipia uanachama bali hii ni kama “happy hour” kwenye pub 😎

Kuna matukio mawili. La kwanza limetokea siku kadhaa zilizopita ambapo mtu mmoja mwenye uelewa wa ndani kuhusu siasa za Tanzania alinielezea kwa kina kuhusu sakata la Tundu Lissu kuvuliwa ubunge.

Nachoweza tu kutamka kwa sasa ni kwamba “tuache muda uongee,” lakini kuna mazito kuhusu ishu hiyo. Mie mtumishi wako ni muumini wa uwazi na ukweli lakini katika hili nitaomba muwe na subra hadi wakati mwafaka kuliongelea kwa uwazi bila kumwaza mtu yeyote.

La pili ni maamuzi ambayo mie mtumishi wako niliyachukua kitambo, kuchukua likizo katika kupiga kelele za siasa. Kama una wasaa soma nilichoandika HAPA

Ugumu wa kuwa mzalendo katika Tanzania yetu una sura mbili, moja iliyo wazi na nyingine iliyojificha. Ya wazi ni hii ambapo ukweli mchungu ni kwamba wengi wenu mmewekeza kwenye vitu visivyo na maana.

Pengine mfano huu unaweza kuwakera baadhi yenu lakini mie ni muumini wa busara kwamba “kuuchukia ukweli hakuufanyi kuwa uongo.” Baada ya kuachana na kelele za siasa huko kwingineko nikajiwa na hili wazo la vijarida, ambalo msingi wake ni immani kwamba MPIGA KURA BORA NI YULE MWENYE UELEWA WA MASUALA MBALIMBALI.

Kwahiyo idea yangu ilikuwa ni kuelimisha kundi la angalau watu 2,000 hivi ambao nao wakielimisha japo watu 10 au 100 au pengine 1,000 tu kwa kila mmoja wao, basi muda si mrefu tungekuwa na kundi si haba la wapiga kura wanaojielewa.

Lakini licha ya zaidi ya watu 1,000 kujitokeza kujisajili kuwa “wanachama wa mkakati huo,” waliokamilisha taratibu rahisi tu za uanachama ni 75 tu.

Kwa ninavyowafahamu Watanzania, hata kufikisha hao watu 75 ni mafanikio makubwa sana, kwa sababu kwa watu wengi “haya masuala ya siasa ni kama yanawapotezea muda.”

Na hapo ndipo Watanzania wengi hawaelewi. Kwamba kutoijali siasa hakuifanyi siasa ikupuuze. Kudai kuwa “ah mie siipendi siasa,” hakumfanyi mwanasiasa mbovu kutofanya maamuzi mabovu yatayoishia kukuumiza.

Image result for quote about politics

Kwa bahati mbaya - au pengine makusudi - jukumu la harakati za kudai stahili za Watanzania zimeachwa mikononi mwa watu wachache. Hadi hapo si tatizo kwa sababu sio rahisi kwa kila mwanachi kuwa mwanaharakati. Tatizo ni kwamba licha ya suala hilo kuwa mikononi mwa watu hao wachache, hakuna sapoti ya maana wanayopata kutoka kwa hao wanaowapigania.

Ni rahisi kujiona mpuuzi hususan unapopatwa na matatizo kutokana na kuwapigania “wanyonge,” huku “wanyonge” hao wakiwa bize na UBUYU na MKEKA/KUBETI. Naam, haya majanga mawili yanakwamisha sana harakati za ukombozi wa Tanzania yetu.

Naomba ieleweke kuwa simaanishi kwamba WATANZANIA WOTE wanaendekeza UBUYU na MKEKA/KUBETI. Hapana. Ila idadi kubwa ya Watanzania akili yao ipo huko.

Sura ya pili ya ugumu wa kuwa mzalendo/mwanaharakati ni jinsi wazalendo/wanaharakati wanavyohujumiana. Ni kama sote twamfukuza mwizi mmoja lakini kila mmoja wetu anataka kuwa wa kwanza kumkamata, matokeo yake twaishia kupigana ngwala wenyewe.

Wakati flani nilianzisha petition kudai haki kwa mamia ya waliouawa huko MKIRU (Mkuranga, Kibiti na Rufiji) lakini jitihada hizo ni kama zilisuswa na “wanaharakati” wenzangu. Na hata nilipovisihi baadhi ya vyama vya upinzani kuunga mkono petition hiyo, hakuna aliyejitokeza - apart from Zitto Kabwe ambaye kimsingi ndiye alini-inspire kuendesha petition hiyo baada ya yeye kuibua mjadala wa MKIRU bungeni.

Kuna unafiki mkubwa tu kwenye “uanaharakati” wetu, ambapo mie mtumishi wako naamini kwa dhati kwamba huwezi kuipenda nchi yetu kama huwapendi watu wako wa karibu/wanaharakati wenzako.

Kilichonisukuma hasa kuandika mada hii ni andiko la mdau mmoja huko Jamii Forums, ambalo nimelipiga “screenshot” japo waweza kulisoma HAPA

Soma bandiko hilo kisha tafakari kuhusu mustakabali wa Tanzania yetu.

Nimalizie makala hii ya wazi kwa tangazo hapo chini ambalo natumaini halitowakwaza msiopenda matangazo.

Uanachama kwa mwaka mzima ni sh100,00 au sh 10,000 kwa mwezi. Tuma mchango wako kwa m-pesa namba 0767632516 (jina Khadija Katule). Kwa walio nje ya Tanzania, unaweza kuchangia kwa KUBONYEZA HAPA.

Ndimi mtumishi wako

Evarist Chahali