Makala Ya Wazi: Musiba Agoma Kuhojiwa

"Maagizo Kutoka Juu" Yaamuru Asibughudhiwe

Mambo ni mengi lakini muda ni mchache. Naomba niruhusu mtumishi wako kuku-update kuhusu yanajiri “chini ya kapeti.”

Taarifa latest zinaeleza kuwa kuna kizaazaa kikubwa kilichozuka baada ya barua iliyochapishwa jana na viongozi wastaafu maarufu wa CCM, Makatibu wakuu wa zamani Yusuph Makamba na Abdulrahman Kinana.

Mtu mmoja anayezielewa vema siasa za CCM amenieleza kuwa Jiwe ameshtushwa sana na uamuzi huo wa Makamba na Kinana ambao mtu huyu ananiambia kuwa ni sawa na “kumpa mchawi mtoto amlee.”

“Kaka, wala sio siri kuwa Musiba anatumiwa na Bwana Mkubwa mwenyewe, kwani hata fungu la Musiba linaidhinishwa Ikulu na Bwana Mkubwa,” anaeleza mtu huyu anayefanya kazi kwenye taasisi moja nyeti (na mmoja wa wazalendo wanaopingana na maovu kwa kunirushia dondoo muhimu hapa na pale)

Inaelezwa kuwa katika masaa 24 yaliyopita, jeshi la polisi lilituma wito kwa Musiba kumtaka aende polisi kwa ajili ya masuala mawili, hizi tuhuma mpya dhidi yake kutoka kwa Makamba na Kinana, na pia kuhitaji maelezo zaidi kuhusu tuhuma alizotoa kuwa watu kadhaa maarufu wanapanga kumuua.

Kwa jeuri kubwa, Musiba amegomea wito huo wa polisi, na baada ya kupokea vitisho “kutoka ngazi za juu,” kila mtendaji wa jeshi hilo anakwepa suala hilo.

Kadhalika, Msemaji wa Serikali Dkt Abbas alipotaka kuchukua uamuzi wa kuyafungia magazeti ya Musiba, alikumbana na kigingi baada ya kutumiwa onyo “kutoka ngazi za juu” kuwa “asimguse Musiba.”

Uamuzi wa Musiba kumvaa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Dkt Modestus Kipilimba kwa kudai kuwa anatoa taarifa za siri za serikali kwa Membe, kumekiweka Kitengo katika wakati mgumu kwa sababu licha ya Musiba kutumia kiwanda cha uchapaji cha Idara hiyo - Malindi Printing Press - na kuwatumia magazeti ya Musiba kutuchafua watu mbalimbali, Musiba amevuka mstari na kumwaga tuhuma hizo nzito dhidi ya Kipilimba. Na kitengo kinafahamu fika kuwa Musiba hakuwa na jeuri ya kufanya hivyo kama si kuhakikishiwa usalama wake na Jiwe.

Japo ni kweli kuwa Kipilimba na Membe ni damu damu, na ni kweli pia kuwa Kipilimba hawezi kuficha kitu Membe, na tuhuma kuwa anampa Membe taarifa ni “siri ya wazi,” Musiba hakuwa mtu sahihi wa kusema hayo.

Naendelea kukusanya taarifa kuhusu songombingo hili ambalo kwa mujibu wa taarifa za kuaminika, tulichoshuhudia hadi muda huu ni trela tu kwani picha kamili yaja hivi punde.

Ikumbukwe kuwa both Makamba na Kinana sio tu ni makada wakongwe wanaojua vema mikakati ya kisiasa, pia wote ni wanajeshi wastaafu, na kwa hakika hawakukurupuka tu na tamko hilo la jana.

Japo wote wanavuna matunda ya mfumo walioujenga, yayumkinika huu ni mwanzo wa jitihada makusudi kuuvunja mfumo huo, na yaelezwa kuwa Jiwe anamini hivyo, which makes him vulnerable - kwa sababu mara nyingi ni mtu anayeendeshwa zaidi na emotions kuliko common sense.

Nimalizie makala hii ya wazi kwa kuahidi updates zaidi, lakini pia kuwashawishi ambao hamjajiunga na uanachama wa #BaruaYaChahali kwamba tunawahitaji huko.

Jinsi ya kujiunga 👇

Uanachama kwa mwaka mzima ni sh100,00 au sh 10,000 kwa mwezi. Tuma mchango wako kwa m-pesa namba 0767632516 (jina Khadija Katule). Kwa walio nje ya Tanzania, unaweza kuchangia kwa KUBONYEZA HAPA.

Endapo unataka kuondolewa kwenye orodha ya wanaotumiwa #BaruaYaChahali JIONDOE HAPA.

Ndimi mtumishi wako,

Evarist Chahali