Barua Ya Chahali

Share this post
Makala Ya Wazi: Majonzi Morogoro Na Tafakuri
www.baruayachahali.com

Makala Ya Wazi: Majonzi Morogoro Na Tafakuri

Evarist Chahali
Aug 12, 2019
7
Share this post
Makala Ya Wazi: Majonzi Morogoro Na Tafakuri
www.baruayachahali.com
Image result for ajali mafuta morogoro

Kabla ya kuingia kwenye mada katika makala hii ya wazi nina ombi: kama wewe ni afisa mwandamizi wa Jeshi la Polisi naomba tuwasiliane (kama unaniamini). BONYEZA HAPA kuwasiliana nami. Thanks in advance.

Twende kwenye mada husika. Wiki iliyopita ilimalizika kwa majonzi makubwa kufuatia ajali mbaya ya moto uliotokana na mlipuko wa gari la kubebea mafuta. Takriban wenzetu 70 wamepoteza maisha yao katika janga hilo. Naomba katika imani yako ya kidini, tuungane kwa dakika moja kuwaombea dua/sala marehemu.

Baada ya dua/sala hiyo, nitumie fursa hii kuwapa pole wafiwa sambamba na kuwatakia majeruhi uponyaji wa haraka.

Wanasema “ajali haina kinga.” Lakini hiyo ya Morogoro sio tu ilikuwa ajali yenye kinga bali inayoepukika.

Kwa upande mmoja, laiti waliokimbilia kwenye gari hilo la kubebea mafuta lililokuwa limepindua wakati huo wangefahamu hatari waliyokuwa wanaikaribia, basi huenda wasingekaribia garihilo na yayumkinika kuamini kuwa kusingetokea kifo japo kimoja.

Lakini kuelewa janga ni kitu kimoja, na “njaa” ni kitu kingine. Ni rahisi kulaumu watu waliohatarisha maisha yao na kwenda kwenye gari hilo ili kupata mafuta. Lakini yayumkinika kuamini kuwa umasikini ulichangia kuwapa ujasiri wa kuhatarisha maisha yao.

Twitter avatar for @ChahaliEvarist Chahali @Chahali
RIP marehemu, pole wafiwa na majeruhi wa janga la mlipuko wa lori la mafuta huko #Morogoro. Ni rahisi kuhukumu na kusema chanzo ni ignorance but root cause is POVERTY. Si wakati mwafaka KULAUMIANA but ni muhimu priority iwe KUPAMBANA NA UMASIKINI badala ya kubinya haki za kiraia

August 10th 2019

21 Retweets108 Likes

Mie mtumishi wako naamini bila shaka kuwa laiti nguvu kubwa inayotumiwa na Jiwe kudhibiti Upinzani na kubinya haki za kiraia ingeelekezwa kwenye kupambana na umasikini, basi hiyo Tanzania ya Viwanda isingeishia kuwa porojo inayotegemea takwimu feki.

Kwa vile vyombo vya habari vimezibwa mdomo - ukichanganya na ukweli mchungu kuwa vyombo vya habari vingi vimesheheni makanjanja wasiojituma kutafuta habari - inakuwa vigumu kufahamu kwa yakini hali ya maisha ni ngumu kiasi gani kwa sasa.

Maelezo mepesi ni kwamba watu walizowea kupiga dili ilhali asilimia kubwa ya Watanzania wapo vijijini ambako hakuna dili yoyote zaidi ya kudhulumiwa na vyama vya ushirika.

Na ukidhani mie mtumishi wako ni mchochezi flani, hata wafadhili wetu wakubwa wanaona mwelekeo wa serikali ya Jiwe sio sawia kwenye masuala ya haki za binadamu/kiraia

Twitter avatar for @ChahaliEvarist Chahali @Chahali
#Norway 🇳🇴 is concerned about the human rights situation in #Tanzania 🇹🇿 which over the past 50 years has received more Norwegian assistance than any other country. https://t.co/u3sXeV9rjUh
Image

August 11th 2019

1 Like

Kwa upande mwingine, jeshi la polisi haliwezi kukwepa lawama kuhusiana na ajali hiyo kwa sababu walipaswa kuweka zuwio ili wananchi wasiingie kwenye eneo lililozuiliwa. Ndivyo ilivyo kwa hawa wenzetu huku pindi kukitokea ajali.

Lakini polisi wetu wanapata wapi muda wa “matatizo madogo kama hayo” huku wakiwa na jukumu kubwa la kuwashughulikia wapinzani? Tuliache hilo!

Kadhalika, kikosi cha zimamoto kilipaswa kuepusha jali hiyo aidha kwa kushirikiana na jeshi la polisi ku-secure eneo la tukio na kufika mapema na kuukabili mlipuko huo baada ya kutokea. Lakini kuwalaumu hawa jamaa ni kuwaonea tu. Licha ya maslahi duni, wanafanya kazi katika mazingira magumu mno wakiwa na vitendea kazi duni. Ni jamb la kawaida kwa gari la zimamoto kufika eneo la tukio huku gari hilo likiwa halina maji ya kuzima moto huo.

Serikali inawekeza vya utosha kwenye magari yenye maji ya washawasha kudhibiti “wakorofi” lakini uwekezaji katika utayari wa kukabili majanga ni mdogo mno.

Huu sio wakati wa kulaumiana, na niliyoandika hapa sio lawama bali kukumbushana vipaumbele na changamoto.

Mwisho ni mshangao wangu kuhusu Jiwe kukacha mazishi ya waliokufa kwenye ajali hiyo.

Twitter avatar for @ChahaliEvarist Chahali @Chahali
#Tanzania: President @MagufuliJP isn't attending the burials (taking place from today) of 60+ people who perished when a fuel tanker exploded yesterday in #Morogoro, about 200km from de-facto capital Dar es Salaam. PM Kassim Majaliwa will represent him instead Strange, isn't it?
Image

August 11th 2019

28 Likes

Nimalizie makala hii kwa tangazo hili hapa chini.

TANGAZO:

Ndimi mtumishi wako

Evarist Chahali

Comment
Share
Share this post
Makala Ya Wazi: Majonzi Morogoro Na Tafakuri
www.baruayachahali.com

Create your profile

0 subscriptions will be displayed on your profile (edit)

Skip for now

Only paid subscribers can comment on this post

Already a paid subscriber? Sign in

Check your email

For your security, we need to re-authenticate you.

Click the link we sent to , or click here to sign in.

TopNewCommunity

No posts

Ready for more?

© 2022 Evarist Chahali
Privacy ∙ Terms ∙ Collection notice
Publish on Substack Get the app
Substack is the home for great writing